MWANAUME anayedaiwa kuwa ni kinara wa ubakaji jijini hapa, Said (30)
mkazi wa Mbauda, amenusurika kifo kwa kipigo kutoka kwa raia wenye hasira baada
ya kunaswa akitoka kumbaka denti wa kidato cha pili hadi kupoteza fahamu.Said
anayetajwa kuwa mwenyekiti wa kundi linalojihusisha na ubakaji, alishambuliwa
na wananchi hao baada ya yeye na wenzake watano kukutwa kwenye nyumba
inayodaiwa kuwa ya uhalifu iliyopo Muriet, Bon City jijini hapa wakimfanyia
kitendo hicho cha kinyama mwanafunzi huyo mwenye umri wa miaka 14 Mashuhuda wa
tukio hilo, akiwemo Mwenyekiti wa Mtaa, Francis Mbise walieleza kuwa mtuhumiwa
huyo akiwa na wenzake hao walimbaka usiku kucha msichana huyo aliyetajwa kwa
jina moja la Jack, mkazi wa Kwamorombo baada ya kufanikiwa kumrubuni kwa maneno
na kumwingiza kwenye nyumba hiyo Baada ya kufanya unyama huo usiku kucha,
alfajiri mtuhumiwa huyo alionekana akitoka ndani ya nyumba hiyo akiwa kifua
wazi na kukimbia, ndipo wananchi walipomtilia shaka na kumkimbiza na baada ya
kukamatwa, aliulizwa kama ni mwizi akakataa bali alitoka kufanya mapenzi na
msichana Mbise alisema kuwa wananchi hao waliongozana naye hadi kwenye nyumba
hiyo na kumkuta msichana huyo akiwa amelala hajitambui huku sehemu zake za siri
zikitoka damu Mwenyekiti huyo alisema walipomuhoji kwa nini alikuwa akikimbia,
alisema yeye alihofu kuwa msichana waliyembaka amepoteza maisha baada ya
kushtuka usingizini na kumwona hajitambui huku wenzake wakiwa Alisema mtuhumiwa
huyo alikiri kuunda kundi la ubakaji lenye watu watano likiongozwa na yeye huku
wakigeuza makazi ya mmoja wa wahalifu hao kuwa danguro la ubakaji. Ndipo
wananchi hao walipoamua kumshushia kipigo cha nguvu kabla ya polisi kufika na
kumuokoa Watuhumiwa wengine walifanikiwa kukimbia na kutotambulika, lakini
wananchi wa eneo hilo wanaendelea kuwasaka.Mtuhumiwa huyo alichukuliwa na
polisi wenye silaha ndani ya gari aina ya Land Rover lenye namba ya usajili PT
1177 huku akiwa ametapakaa damu usoni
BINGWA WA KUBAKA ANUSURIKA KIFO
KIJANA Said akipata huduma ya kwanza baada ya kupokea kichapo kutoka kwa wananchi wenye hasira kali