Idadi kubwa ya watu walifurika barabara angalau kumtupia jicho shujaa
wao na kutoa heshima zao za mwisho. Takriban watu 100,000 walitoa heshima zao
za mwisho kwa Mandela mjini Pretoria siku ya Ijumaa kabla ya mamia ya wengine
kukosa fursa hiyo pale walipokatazwa kumuona Mandela kutokana na ufupi wa muda.Mandela
aliyefariki tarehe tano Disemba atafanyiwa maziko ya kitaifa siku ya Jumapili, Kijiji
cha Qunu
Kijiji cha Qunu ambako atazikwa Hayati Nelson Mandela, kinaomboleza kifo
cha shujaa aliyetoka katika kijiji hicho Nelson Mandela. Mazingira hapa ni ya
kipekee, mchanganyiko wa nyumba za kisasa na za kitamduni ambazo mfano wake ni
mizinga ya Nyuki.
Visima vya maji anavyovikumbuka Mandela bila shaka hawezi kuviona sasa.
Lakini viwanja vya kijiji hiki viko chini ya majabali ambayo yeye na rafiki
zake walikesha wakichezea.
Ni viwanja hivi ambapo Madiba alijifunza kuwinda Ndege , kuchukua asali
misituni na matunda ya misitu ambayo ilikuwa inaliwa wakati huo.
Alipokuwa na umri wa miaka 5, Mandela aliandika kumbukumbu zake kuhusu
safari yake alivyopigania uhuru wa Afrika Kusini, pia alijifunza kuchunga Ng’ombe,
na kupitia kwa kazi hiyo alijifunza uhusiano uliopo kati ya watu wa kabila la
AbaTembu na Ng’ombe wao.
Alisomea hapa Qunu, lakini kijiji alichokiacha kwa huzuni wakati
alimzika babake kimebadilika. Lakini aliporejea hapa mwaka 1990 alipokuja
kutembelea kaburi la mamake , alisema aliona umasikini mkubwa machoni mwa watu
wa Qubu, viwanja visafi alivyovikumbuka havikuwepo tena, vilikuwa vimejaa
takataka kitu ambacho hakuwahi kukiona tangu alipokuwa mtoto.
Hata hivyo Kijiji cha Qunu bila shaka kimebadilika pakubwa, ni kisafi
kikubwa na kina dalili za maendeleo, wala sio taswira aliyoitoa Mandela katika
kumbukumbu zake kuhusu nyumbani.
Na sababu moja ya hilo ni kuwa alijenga nyumba hapa pamoja na shule,
alileta maji, umeme, pamoja na mapato kwa watu wa eneo hili kutokana na makazi
aliyojengewa Mandela ambako atazikwa.