NA SKY BONGO, Morogoro.
HII ni kipande cha sababu chenye umbo mfano wa simu ya kiganjani ambacho hutumika kuwaibia watu pale mitaa ya Sabasaba kuanzia jumatatu hadi jumapili kwa maana ya siku saba za wiki na vijana wanaotumia fursa ya kumwona mtu anayeonekana kwa macho ni mshamba pindi anapopita katika anga zao.
Eneo la barabara ya Sabasaba ikitumiwa na usafiri wa umma maarufu kama daldala za Mzumbe, Mlali na Chamwino N:K, eneo hilo limekuwa hatari sana hasa wanawake na wanaume wenye muonekana huo wa ushamba ushamba ambao hao ndio waathirika wakubwa sana na matukio ya kupora simu, kuchaniwa viwembe beki zao na kuchukuliwa fedha hata kama watakuwa wamestukia mchezo huo kutoka kwa vijana wenye makazi yao Manzese Manispaa ya Morogoro.
Hii ni bahasha ya kaki ndani yake huwekwa kipande cha sababu chenye umbo la simu.
JE UNAIBIWAJE AMA UNAPORWAJE VIP SIMU NA FEDHA ?.
WIZI wa fedha kutumia simu ya sabuni ya nche imekuwa ikiwakumba watu wanaonekana kama ni washamba hasa wanaume au wanawake wamekuwa wakilazimishwa kununua simu halisi kisha mteja anapochukua fedha kutoka mfukoni (WIZI) hubadilisha simu halali na kuchukua bahasha yenye kipande cha sabuni ya nche iliyoweka vizuri katika bahasha ya kaki na tendo hilo hufanyika kwa haraka sana wakati mteja wake anachukua fedha kutoka mfukoni ama katika mkoba.
MWIZI
Huwa na bahasha mbili katika mifuko yake ya suruali ya nyuma moja ina kipande cha sabauni ya nche na nyingine inakuwa haina kitu, sasa basi kinachoendelea wakati mteja anachukua fedha kutoka mifuko ama katika mkoba kiujumla akili yoye ina hamia katika kuchambua fedha na kipindi hicho na yeye hutumia kukubadilishia simu halisi na kukuwekea kipande cha sabuni.
MIKOPA AMA POCHI KWA AKINAMAMA.
Wanawake wenye mabegi au mapochi wamekuwa wakichaniwa viwembe na vijana hao na kama itashindikana zoezi hilo la kuchana mabegi hutumia njia rahisi kwa ya kukwapua pochi na kukimbia nalo wakitokemea mitaa hiyo hiyo ya Manzese huku wenye maduka na wapita njia wengine wakiangalia tukio hilo bila kutoa msaada wowote.
ENDAPO MUATHIRIKA.
Endapo muathirika wa tukio hilo atathubutu kumfuata ama kuwafuata atakumbana na adha ya kupigwa na kundi la vijana ambao wapo katika kundi hilo na pengine kuporwa na mali nyingine watakazoona zinafaa kwao na wakati huo uwe umejiandaa kuumia kwani watakushambulia kwa kila aina ya mashambulio watayoona wao yanafaa kukushambulia ili usiendelee kuwabughuzi.
BARABARA YA SABASABA IMEKUWA HATARI.
Kando ya barabara ya Sabasaba eneo la kuingia kanisa kuu la Anglikana hadi kona ya maegesho magari yaendayo Mzume na Mlali imekuwa hatari kwa watu wenye muonekano wa kishamba ama kuzubaazubaa (sio wachangamfu katika sura zao) ndiyo watu wanaokumbwa zaidi na matukio ya kuibiwa kwa mfumo huo kwani wamekuwa warahisi kwao pindi wanapotekeleza uhalifu wao tofauti na mtu anayeonekana kama ni mjanja kwa maana watasumbuana naye katika uporaji.
JE WAHUSUKA WENYE MAMLAKA YA KULINDA USALAMA WA RAIA NA ZAKE MNAIJUA HII KERO ?.
Imekuwa kero kubwa sana kwa akinamama na wanaume wenye muonekana wa kishamba (sijapata kiswahili bora cha kuwaita) muweze kuwanusuru na atha hii ambayo naamini inaweza kudhibitiwa kwa haraka ili kundi hili liondokane na unyonge wa manyanyaso.
Ukiachilia mbali kundi hilo pia huwakumba hata wanafunzi wanaoonekana wanaweza kumiliki simu na kujikuta wakiingia katika mtego wa vijana hao, ambapo bei za simu halisi huwanadisha kwa bei ya sh30,000 hadi sh5,000 pindi wanapoona pesa ipi huwa hawaachi kitu.
Ushauri wangu:
Kundi hili limekuwa kero kubwa sana Manispaa ya Morogoro, hasa eneo hilo la Sabasaba, je ukifanyika msako wa kimpya kimpya kwa maana ya kuwakamata na kupewa adhabu ya kufanya usafi japo katika maeneo ya ofisi za serikali ambako sehemu nyingine zinahitaji usafi wa kila siku waharifu wa namna hii hawawezi kupewa adhabu hiyo ?.
Tufikie wakati sasa wenye mamla kuangalia mbele katika masuala mbalimbali ndani ya jamii hasa kwa kuondoa kero zinazowagusa raia moja kwa moja nafikiri hata hao wenye haki za kutetea haki za binadamu muwashirikike tuone mchango wao katika kero ndani ya jamii, mimi sidhani kama wataendelea kupinga kila jambo ambalo litahitaji kutatuliwa maana kama hajaibiwa yeye atakuwa ameibiwa mtoto wa shangazi yake ama kaka yake N:K.
HABARI HII IMEFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA NDANI YA SIKU 7 ZA WIKI KWA ZAIDI YA MWAKA HUKU JUMAMOSI NA JUMAPILI HUWA VITENDO HIVYO HUJITOKEZA ZAIDI NA HIYO INATOKANA NA WATU WENGI KWENDA KATIKA MNADA WA KIKUNDI NA SABABU WAKITUMIA KANDO YA BARABARA HIYO NA WAO WAKINUFAIKA ZAIDI KUFANYA UHALIFU.
HILI LINAWEZEKANA ENDAPO TUTAAMUA NA KUTOKOMEZA.
CHANZO:SKYBONGO BLOG