Je Wanaume wa Aina hii Wanaweza Kuwa watunzaji Wazuri wa Familia?
Nina jambo ambalo nimekuwa nijiuliza sana na kutafutia majibu bila kujua majibu sahihi ni yapi hasa na hivyo kuamua kulileta swala hili humu mmu.
Swala lenyewe ni hili:
Unakuta binti yuko kwenye uchumba kwa muda mrefu,lakini anakuambia mchumba wake(mwanume )hajawahi kumnunulia chochote kama zawadi na kumpa,mpaka binti mwenyewe aombe ndipo anunuliwe na kupewa kitu hicho na huyo mwanume anadai kabisa kuwa anampenda sana na yuko tayari kufunga naye ndoa na anatoa ahadi kuwa atamtunza chini ya hali yoyote.maswali yanakuja hapa:
1.kama ameshindwa japo kununua kitu chochote hata ikiwa ni cha thaamni ndogo sana na kukupa wakati wa uchumba?je atakapokuoa anaweza kukutunza kwa mahitaji yako yote?
2.tabia kama hiyo huashiria nini?ubinafsi?au mtihani aone ikiwa kwa kweli hupendi vitu au pesa zake ila unampenda yeye?
3.je kuna uwezekano kuwa anaweza kuwa hivyo kwenye uchumba lakini akawa mtunzaji mzuri wa familia hapo baadaye bila kuombwa afanye hivyo?
4.je mwanume wa aina hiyo aweza kuwa mtunzaji mzuri wa familia,au ndo mpaka akumbushwe,hatuna hiki leo,hatuna mboga,mume wangu ada ya watoto,mume wangu naomba hela ya khanga nimeishiwa?
Najua kwa kipindi cha sasa majukumu ni kusaidiana,lakini ukweli utabaki pale pale kwamba mume ndiye mtunzaji mkuu wa familia na wala hawezi kutegemea kipato cha mke ndio kitunze familia.
Wana mmu naombeni michango yenu katika hili,wote wanawake kwa wanaume,najua wapo ambao hawamo ndani ya ndoa lakini wana uhusiano na watu wa aina hii na wapo ambao walikuwa kwenye uhusiano na watu wa aina hii na sasa wameshafunga ndoa na wanajua jinsi ya kushughulika nao,hivyo kupita michango mbali mbali humu wote tutafaidika,wenye uzoefu tunaomba uzoefu wenu na hata msio na uzoefu tunaomba maoni yenu mnaonaje hali kama hii.