KITUKO!! MPANGAJI NA WAFANYAKAZI WAKE WAFUNGIWA NDANI DUKANI KWA KUCHELEWA KULIPA KODI



Katika hali isiyokuwa ya Kawaida Shirika la Nyumba la Taifa(NHC) Mkoa Mbeya limemfungia mpangaji wake ndani ya duka katika kile kilichodaiwa kuchelewa kulipia pango la chumba hicho kwa muda uliokusudiwa ambao ni Mwanzo wa Mwezi
Tukio hilo ambalo lilivuta hisia za Watu
wengi kutokana na afya ya Mpangaji huyo anayesumbuliwa na Kisukari kwa Muda mrefu limetokea Leo majira ya saa nne kati kati ya Jiji la Mbeya ambapo Watumishi wa Shirika hilo walifunga Duka la Kuuzia vifaa vya Maofisini(Stationery) inayojulikana kwa jila la Rubi iliyopo Posta.

Mzee BonifaceIshabakaki(Lubi), na Cecilia wakiwaonesha waandishi wa habari majina yao kuptia dirisha lakioo wakiwa wamefungiwa na shirika la nyumba.


Akizungumzia
Dirishani kufuatia kufungiwa kwa duka lake na yeye akiwa ndani pamoja
na wafanyakazi wake wawili, Mmiliki wa Duka hilo, Boniface Ishabakaki,
alisema ameshangaa kufanyika kwa kitendo hicho kwa sababu tayari Mke
wake alikuwa ameshaongea na Meneja na kumtumia Fedha kwa njia ya Mpesa 
tangu saa nne lakini alivyowaeleza walishindwa kumuelewa.



Afisa wa shirika la Nyumba mkoani
Mbeya, Alfan Chaula, baada ya kufungua kufuli  akiwa anawakwepa wana habari

Afisa wa shirika la Nyumba mkoani
Mbeya, Alfan Chaula, baada ya kufungua kufuli  akiwa anawakwepa wana habari

Mmiliki wa Duka hilo, Boniface Ishabakaki, akiongea na waandishi wa habari baada ya kufunguliwa duka lake



upande wakeKaimu Meneja wa shirika la Nyumba mkoa wa Mbeya S.C Katanga
amesema Ndugu Ishabakaki ni mpangaji wao wa nyumba Na. 003 Kiwanja Na.
6/3 Mtaa wa Lupaway. Mbali na jitihada zote za kumdai kodi amekuwa
msumbufu kulipa pia historia yake ya ulipaji kodi si mzuri hata
kulifikisha shirika katika hatua ya kutoa Notisi na wakati mwingine


Hata hivyo baadhi ya watu walioshuhudia
kitendo hicho wamelaani vikali kwa kile walichodai Shirika hilo limegeuka adui
wa wapangaji wao ambao hata hivyo hawana madeni ya kutisha na siyo wasumbufu
kwenye ulipaji na kuongeza kuwa mzee huyo amekuwa mpangaji wa shirika hilo
tangu Mwaka 2000


Amos Manyama Afisa Miliki wa shirika la nyumba akielezea mikakati ya shirika hilo kwa waandishi wa habari

Socials