MCHAWI AUAWA NA WANANCHI DAR ES SALAAM

Maskini anatia huruma kweli

WANANCHI wenye hasira kali wamempiga
hadi kumuua mtu mmoja mwanaume aliyesadikiwa kuwa ni mchawi baada ya
kuanguka akiwa amepanda ungo maeneo ya Mbezi Luis jijini Dar es Salaam
Kijana huyo mkazi wa Mwanza
anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 20 hadi 25, alianguka jana
saa 12 asubuhi maeneo hayo baada ya kudai kuwa alikuwa kwenye safari
zake za kishirikina



 Kabla ya kufariki alisema ;mimi nilikuwa na wenzangu sita, wanaume watatu na wanawake watatu ambapo tulikuwa tunatoka Mwanza kuelekea kwenye mkutano wetu
Lakini mimi kwa bahati
mbaya nilikiuka masharti tuliyopewa na mkuu kwa kufungua macho ndipo
ghafla nilianguka na kupata kadhia hii inayopelekea mauti yangu

Hata hivyo kutokana na
vurugu zilizokuwapo eneo hilo la tukio, ambapo wananchi wa
eneo hilo walikuwa wanataka kumuua, kijana huyo alishindwa hata kutaja
jina lake kutokana na kipigo alichokuwa anakipata kutoka kwao
Kwa mujibu wa mashuhuda
wengine wa tukio hilo walisema baada ya kuanguka eneohilo walimkimbiza
hadi ndani kwa mtu na kumtoa pamoja na zana zake za kichawi ambapo
walizichoma kwanza moto ikiwa pamoja na ungo wenyewe ndipo wakaendelea
kumpiga kwa mawe hadi mauti yalipomkuta.
Huyu jamaa bwana,
ameanguka hapa, sasa kwakuwa sisi hatuna mzaha na watu kamahawa
tumemtoa huko alikokimbilia na kumhalalisha kwa vijana wa kazi hapa
baada ya kuhakikisha zana zake zote tumezichoma moto alisema mkazi
mmoja wa maeneo hayo
Sisi tumepiga simu kituoni
hapo hata kabla huyu mchawi hajaanza kushambuliwa, lakini angalia
tukio limeanza saa 12 asubuhi wanakuja baada ya masaa mawili, huu nu
uzembe” alisema mkazi wa eneo hiloaliyejitambulisha kwa jina moja la
Ali
Mtanzania lilibisha hodi
katika kituo cha Polisi Kimara ambacho mwili wake ulipelekwa ili kupata
uthibitisho zaidi lakini askari wa zamu waliokuwa mapokezi walisema
hawana mamlaka ya kutoa maelezo hadi mkuu wa kituoa au mkuu wa makosa ya
kieupelezi wa kituo hicho ndiyo wenye dhamana.
Aidha wakuu hao OC CID
(ASP) M. Mganga pamoja na Mkuu wa kituo wote hawakuwapo kituoni wakati
Kamanda wa kipolisi wa Kinondoni, Elias Kalinga hakuweza kupatikana ili
kudhibitisha tukio hilokutokana na namba yake ya simu kuita bila
kupokelewa


Socials