Usafiri wa Krismasi majanga UBT

Usafiri wa Krismasi majanga UBT


Dar es Salaam/Moshi. Mamia ya abiria, wamekwama kusafiri katika Kituo Kikuu cha Mabasi yaendayo mikoani na nchi jirani cha Ubungo  jijini  Dar es Salaam kutokana na upungufu wa mabasi.
Abiria hao pia wamelamikia  ongezeko kubwa la nauli ambazo sasa zimefikia Sh70,000 kutoka Sh23,000 kwa mabasi ya kwenda katika Mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Mbeya na Iringa.
Imeelezwa kuwa pamoja na maofisa wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra) kuweka kambi kituoni hapo, lakini wameshindwa kukabiliana na hali hiyo.
Ofisa Leseni wa Sumatra, Sebasitia Lohay alisema ongezeko la abiria kipindi hiki cha sikukuu ni la kawaida na kwamba hakuna tatizo la usafiri.
“Hakuna tatizo la usafiri na ni kawaida kuwa na idadi kubwa ya abiria katika kipindi hiki…tunaendelea kukagua nauli na kuwatoza faini watakaobainika kupandisha nauli,” alisema Lohay jana asubuhi.
Mwananchi iliyokuwepo kituoni hapo mapema asubuhi, ilishuhudia abiria wengi wakiwa hawafahamu cha kufanya baada ya kukosa usafiri.
Pia, Mwananchi ilishuhudia mabasi aina ya Coaster yakiwa yamejaa abiria wanaokwenda Mikoa ya Kilimanjaro na Arusha.
Wakizungumza na waandishi wa habari hizi kwa nyakati tofauti, abiria hao walikiri kuwa hali ya usafiri katika kituo hicho ni mbaya na kwamba upungufu wa mabasi umesababisha ongezeko la nauli hadi kufikia Sh70,000.
Tatizo la upungufu wa mabasi na kuongezeka kwa nauli za mabasi katika Kituo cha Mabasi cha Ubung0, linajitokeza kila mwaka na kusababisha malalamiko kutoka wananchi wanaotaka kusafiri ili kwenda makwao kusherehekea sikukuu.
Baadaye, tatizo hilo linawakumba wananchi hao katika mikoa yanayokwenda na mara kadhaa wanalazimika kusafiri kwa malori kurejea jijini Dar es Salaam.
Mkesha wa Krismasi
Mkesha wa Sikukuu ya Krismasi utafanyika leo kitaifa kwenye Kanisa Kuu la AIC (Africa Inland Church) mkoani  Geita.

Socials