Mi nimetoka mtaa wa pili hapo nshazinguana na mademu flani walikuwa wanataka kuniletea za fesibuku nikawashtukia, nikawachana, wamemaindi nikaona isiwe tabu, nikaachana na kibaa chao ikabidi nije maskani tupige stori.
… Inakuwaje kwanza?
Uko fresh?
Us’konde wala nini mwanangu, naona kama nataka kukuzingua vile, mi leo amani tu hapa, na sikuulizi mambo ya mwaka unaoisha najua ulizingua watu sana mwaka huu, acha uende tugange yajayo.
Uongo?
Najua unaitaka hii stori ya mademu niliozinguana nao mwanangu, ntakupa ila kwanza ngoja niwarushe wanangu wanaonisoma deile ambao mwaka umeisha huku wakiendelea kunipiga tafu, kwa kulifuatilia Zee kila linakokatiza.
Mwanangu Eddy Seng wa Mabegi bila nauli, Fisi, Rioba, Makunga, hata wewe pia mwanangu Big Up, mwaka ushasepa, tugange yajayo.
Sasa hao mademu bwana mi siyo kwamba walikuwa washkaji zangu wala nini, walikuwa ni watu tuliokutana nao fesbuku humu, kila siku wananizingua mara Ooh, ..Zee ibuka kiwanjani kwetu tule gambe na nini ... Mi nikawa nawakata stimu tu kwa kuwapigia stori za waifu.
...Si unajua zile...
Unafkiri wanakoma sasa, wakawa kama wanakomaa tu hivi kwa kuweka picha zao za kujiseksisha, mara tutoke nini, sasa kila nikiwaangalia nikawa kama nazimika hivi, watoto wakali kweli ujue?
Siku moja mtu mzima nikaona kwani nini? Siyo kesi, ngoja nikajimiksi na watoto wazuri na mimi nioshe vumbi, ingawa kiukweli mtoto mkali kuliko wote ni waifu wangu na ndiyo maana yuko homu pale.