Hivi Huyu Halima Kimwana ni Nani Kwa Diamond?
Kuna watu wanashangaza kidogo,siyo kwamba tunawafuata majumbani mwao na 
kugundua tabia zao,kwamba wanakula sana,wachoyo,wachafu au hawapatani na
 majirani zao,hapana,wanayoyafanya ama kuzungumza,wanatufanya 
tuwatambue.Lakini tunaishia kuwajua kwa majina na matukio yao.Ukiniuliza
 babu Tale ni nani,fasta nitakujibu kuwa ni msaidizi wa shughuli za 
Diamond,Romie Jones nitakuambia ni ndugu yake Diamond,Wema Sepetu,ni 
usingizi wa Diamond,kwa maana ya mpenzi,lakini ukiniuliza Halima Kimwana
 ni nani,naweza kulipuuzia swali lako kwa maana sitambui wala kujua ni 
nani kwa Diamond.
Siwezi kuacha kujiuliza hivi huyu binti wa mjini  ni nani kwa 
Diamond?rafiki,dada,shemeji yake,mpambe au nani,Au ndiye kiunganishi 
chake kwa wale viumbe waliosababisha aitwe sukari ya warembo?yeye ni 
nani haswa hata afikie hatua ya kumchagulia Diamond mpenzi wa kuwa 
nae,ni nani hasa hata afikie kumaindi uwepo wa Wema kwenye himaya ya 
Diamond,kajina kake kamezidi kukaa on ea kwa kipindi kirefu kutokana na 
uwepo wake karibu na Diamond,ana nguvu sana kwa Diamond,Nilipuuzia kwa 
muda mrefu sana nikiamini ni mtu wake wa karibu wa kumshikia poda awapo 
lokesheni ya video zake,au anashikilia simu zake awapo stejini,baadae 
nikadhani kuwa huenda ni msaidizi wa mambo binafsi ya Diamond.Lakini 
kufikia hatua ya kumpangia Diamond mwanamke  wa kuwa nae,kidogo hapo 
nashindwa kuelewa,yeye ni nani kwa Diamond?
Wadau mnaojua uhusiano wa huyu dada hebu mtujuze,ni nani,anafanya 
shuhuli gani,naamini wote mliosoma gazeti hilo mna kiu ya kujua.