NDEGE YA ETHOPIA AIRLINE ILIVYOCHIMBA UWANJA WA NDEGE ARUSHA BAADA YA KUTUA GHAFLA IKIWA NA ABIRIA 200
Ndege aina
ya Boeing 767 inayosadikiwa kuwa ni ya Shirika la Ndege la Ethopia imetua kwa
dharura majira ya saa tisa alasiri katika kiwanja cha kurushia ndege ndogo cha
Arusha badala ya kiwanja cha ndege cha
kimataifa cha Kilimanjaro, KIA. Abiria waliokuemo ndani ya ndege hilo takriban
200 wamenusurika kufa baada ya ndege hilo kutua kwa dharura na kupitiliza nje
ya uwanja na kuchimba shimo.