Diwani wa
Kata ya Kisesa (CCM), Clement Mabina (56), amezikwa mchana huu
shambani
kwake Kanyamati, Kisesa mkoani Mwanza. Mazishi hayo yamehudhuriwa na Waziri wa
Ujenzi, Dk. John Magufuli, Waziri wa Nchi
Ofisi ya
Rais (Mahusiano na Uratibu), Stephen Wasira, viongozi wa
serikali,
madhehebu ya dini, vyama vya siasa, wananchi na wakazi wa
Kisesa ambao
wameungana na ndugu, jamaa na marafiki kumsindikiza
marehemu
Mabina. Mazishi hayo yalitanguliwa na ibada iliyofanyika uwanja
wa Ngomeni-Kisesa, Mwanza