“Kwa mfano, tendo la ndoa linaondoa msongo wa mawazo iwapo unayetenda naye unampenda na amekupa maandalizi mazuri. Sidhani kama alimradi utende hilo tendo na yeyote litakusaidia,” anasema mtaalamu huyo.
IINGAWA tendo la ndoa lisipofanywa kwa kuzingatia kanuni na taratibu, sambamba na umakini, linaweza kusababisha maradhi, lakini kwa wanandoa, tendo hilo linatajwa kuwa na manufaa mengi kiafya tofauti na faraja ya kawaida iliyozoeleka kwa wengi.
Imefahamika kuwa tendo hili likifanyika ipasavyo husaidia kuondoa msongo wa mawazo, maradhi ya moyo, maumivu ya kichwa yasiyokoma na kupunguza kasi ya saratani ya tezi dume.
Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Sayansi ya Tiba Muhimbili (Muhas), Dk Yahya Kishashu anasema inategemea tendo linafanywa na nani na mhusika yupo kwenye mazingira gani.
“Kwa mfano, tendo la ndoa linaondoa msongo wa mawazo iwapo unayetenda naye unampenda na amekupa maandalizi mazuri. Sidhani kama alimradi utende hilo tendo na yeyote litakusaidia,” anasema mtaalamu huyo.
Anaongeza kuwa ndiyo maana baadhi ya watu wanatoka nje ya ndoa zao kwa sababu si mara zote tendo la ndoa linawafurahisha wanandoa.
“Wakati mwingine tendo hilo laweza kuwa karaha kwao,” anasema