DIAMOND ACHEFUA WAISLAM..ACHEZA NGOLOLO MAULIDINI

DIAMOND ACHEFUA WAISLAM..ACHEZA NGOLOLO MAULIDINI

KIJOGOO wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ amewachefua waumini wenzake wa Kiislamu baada ya kutupia swaga za staili ya Ngololo kwenye shughuli ya Maulidi.
Tukio hilo lililowagusa waumini hao lilitokea juzikati ambapo kulifanyika Maulidi ya kumtoa nje mtoto wa dansa wake aitwaye Moze Lyobo maeneo ya Mbagala, jijini Dar.

Awali watu waliokuwepo eneo hilo walifurahia uwepo wake lakini kadiri walivyoaanza kugundua kasoro ndipo mambo yalipoanza kuharibika.

“Watu hawakumshtukia, lakini walipomkagua kwa makini na kugundua licha ya kuvaa mavazi ya
Kiislamu ndani yake ana macheni ya dhahabu shingoni kitu ambacho dini hairuhusu,” kilidai
chanzo baada ya mwandishi wetu kufika eneo la tukio na kukuta shughuli imeisha.

Kama hiyo haitoshi, ikaelezwa kuwa Diamond alizidi kuchafua hali ya hewa baada ya kucheza
staili ya Ngololo kwenye kaswida kitu ambacho kiliwashangaza wengi.

“Mwanzo alianza vizuri lakini kadiri dufu lilivyokuwa linakolea, akawa anajisahau na kucheza
Ngololo, kimsingi aliwaboa baadhi ya Waislamu waliokuwa pale,” alisema shuhuda wetu.
Hata hivyo paparazi wetu alitonywa kuwa, baada ya kucheza sana, Diamond alichoka huku jasho
likimchuruzika ambapo aliamua kupumzika na kuwaacha wengine wakiendelea.

BOFYA HAPA UPATE ZINGINE KALI ZAIDI

Socials