FAIDA ZA WABEBA MABOX WAISHI NCHI ZA NJE KAMA UK KWA UCHUMI WA TANZANIA


wabeba boksi ni wa Tanzania wanaoishi ughaibuni, wakifanya kazi za mikono, kama vile kubeba na kupanga mizigo ya bidhaa madukani, kusafisha maofisi, kusafisha vyombo mahotelini, kuwatunza wazee, na kadhalika. Watanzania wanaposema kubeba boksi, wanamaanisha kazi za aina hiyo. Na jina hilo linatokana na huu kweli kuwa wengi wa wahusika wanabeba na kupanga maboksi.

Wabeba boksi wanataniwa sana katika jamii ya kiTanzania. Wabeba boksi wengi nao wanajitania. Watanzania wengi wanaziona kazi za boksi kuwa ni kazi duni. Napenda kubadili mtazamo huo kwa kuelezea umuhimu wa boksi. Natumia hilo neno boksi kwa sababu linatumika pia kumaanisha kazi ya kubeba boksi.

Jambo moja la msingi ni kuwa wabeba boksi wanatumia nguvu zao kujipatia kipato. Wao ni tofauti na wezi au mafisadi, ambao wanakula jasho la wenzao. Kwa msingi huu, mbeba boksi anastahili heshima.

Kila kazi halali ina umuhimu wake katika jamii, iwe ni kilimo, uvuvi, usafishaji vyoo, ualimu, udaktari, au upigaji muziki. Kila kazi ya aina hiyo inastahili heshima. Mpiga boksi anafanya kazi muhimu. Bila yeye, jamii itakwama. Anastahili heshima.

Wabeba boksi, kama vile walivyo waTanzania wengine wanaoishi ughabuni, wanatoa mchango mkubwa katika kipato cha Taifa, kwa hela wanazotuma nyumbani, iwe ni kwa ndugu, jamaa, marafiki, au taasisi. Nimesoma taarifa kuwa mwaka 2008, kwa mfano, watu hao waliliingizia Taifa dola zaidi ya 100 millioni. Wenzetu waKenya wanaoishi nje waliingiza nchini mwao dola zaidi ya 400 millioni. Ni wazi kuwa mbeba boksi, akiwa ni mmoja wa watu hao, ni mtu muhimu kwa uchumi wa Taifa. 

Je, lipi bora zaidi: kukaa vijiweni nchini bila ajira, au kubeba boksi? Hili ni suali la kutafakariwa.

Kuna wabeba boksi ambao, baada ya kukusanya hela, wanaanzisha miradi nyumbani wakiwa bado ughaibuni, na wengine wanarudi nyumbani na kuanzisha hiyo miradi. Kwa njia hiyo, wanatoa ajira kwa wananchi wenzao.

Mpiga boksi, kwa kukaa ughaibuni, anajifunza mengi. Anarudi nchini akiwa na upana wa mawazo kuhusu dunia na uzoefu wa nidhamu ya kazi, vitu ambavyo vinaweza kutoa changamoto kwa wananchi wengine.

Kwa ufupi, boksi lina umuhimu na heshima yake.

ngoja. niwape mfano mnaweza na nyie kufungua
www.diasporamessenger.com/kenyans-abroad

kenyans living abroad sent back home ksh 110.76 billion. ( $ 1.29 billion) na hii ni mwaka jana pekee hizo ni zaidi ya Trillion 1 za Tz

Socials