FAHAMU MANENO HAYA YA MSINGI KATIKA FACEBOOK


Poke:  Neno hili linamaanisha kuwa ni kutoa salamu ya juu juu kwa mtu husika ambaye unampoke. Na pia kinachotokea ni kuwa kama huyo mtu atakupoke pia kurudishia poke yako ni kwamba hata kama sio mmoja wa Friends wako,  basi unakuwa umemruhusu awe na uwezo wa kucheki wasifu wako (profile) yako. Kwani mara nyingi kama mtu sio rafiki yako,  na ume iset profile yako watu wasione profile yako hawawezi kuiona, ila kwa kujibu  poke ya mtu asiye rafiki yako, unampa nafasi ya kuona profile yako, na wewe pia waweza ona profile yake. 

Fans: Kama una ukurasa maalum wa FB, tunaita Facebook Page, basi wale ambao wame LIKE ukurasa huo ni fans wako. Yaani washabiki au watu wenye kuupenda huo ukurasa.

Friends:  Kama una akaunti yako binafsi basi wale ambao wanatajwa kwenye wasifu wako kama Friends hao ndio waweza kuwaita friends.  Kitendo cha kuongeza friends wako wa FB tunasema  una ADD friends.

Members: Kuna makundi mengi katika FB unaweza kujiunga. Basi wale ulionao pamoja kwenye kundi husika ni wana kikundi wenzako, au tunaita MEMBERS. Haipendezi kuita waliojiunga na kundi lako kuwa ni FANS.

Tagging : Unapomtag mtu mwingine iwe picha au status tuu ya maandishi ina maana kuwa unataka yafuatayo yafanyike : Kwanza picha hiyo ionekane kwenye akaunti ya huyo mtu kana kwamba huyo mtu aliweka picha hiyo. Pili unataka rafiki za huyo unayemtag waone hiyo picha.

Hashtag: Unapotumia alama hii #  ni kwamba unataka post husika ijumuishwe kwenye kundi la posts nyingine ambazo pia zimetumia neno ambalo wewe umetumia na hiyo #.  Mfano kama umeandika status kisha ukaweka kama hivi #specialone basi  ukibofya hilo neno special one kwenye status yako utaona utaletewa mjumuiko wa posts nyingine zilizotumia hilo neno. Angalia mfano pichani hapo chini.


Follow: Juu ya profile ya rafiki yako utaona neno Follow au Following . Utaona neno Follow kama haujachagua ku follow, na kama umechagua basi utaona inaonyesha Following. Maana ya neno hilo ni kuwa unachagua kufuatilia posts zake huyo mtu kwani inawezekana mtu akawa rafiki yake ila usiamue kufollow hivyo hautoona posts zake.

Subscribe: Mara nyingi utaona neno hili juu ya profile ya mtu ambaye tayari amefikisha kikomo cha idadi ya marafiki anaoweza kuwa nao FB, au ameamua kuset hiyo button ionekane kwa profile yake.

Socials