Gaidi wa Kitanzania Aliyekamatwa Nchini Kenya Kwenye Tukio la Mauaji Garissa Ahojiwa


Mtanzania mmoja ambaye alikamatwa kuhusiana na shambulio la kigaidi katika Chuo Kikuu cha Garissa, Kenya (jina linahifadhiwa) ahojiwa.

Taarifa zilizopatikana juzi usiku na kutangazwa na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), zilieleza kuwa Mtanzania huyo alihojiwa kuwapo kwake katika eneo hilo hasa ikizingatiwa kwamba siyo mwanafunzi wala mtumishi katika chuo hicho.

Taarifa hizo zinasema kuwa Mtanzania huyo ni miongoni mwa watu wanne waliokuwa wamejificha katika mabweni ya chuo hicho na kati yao, wawili walibainika kuwa ni wanafunzi.

Baada ya kuhojiwa akakiri kuwa wamepanga kufanya shambulio kubwa nchini Tanzania katika Tamasha la Pasaka lilopangwa kufanyika tarehe 05/04/2015 Dar es salaam.


Hata hivyo, Msemaji wa Jeshi la Polisi, Advera Bulimba alipoulizwa jana kuhusu Mtanzania huyo,alikiri hayo na kusema bado wamemuweka chini ya ulinzi kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Socials