VIJIMAMBO: Simu ya Mwanaume Naiona Kama Bomu-Lulu




Siku hizi sio kitu cha ajabu kusikia au kuona wapenzi wamegombana na kufikia hadi kuachana kisa simu za mikononi. Wapo wanaoishi kwenye dhana ya simu ya mkonomni ya mpenzi wako ni simu yako na wapo wanaoishi kwenye dhana ya kila mtu na simu yake na mambo yake hakuna kuchunguza simu ya mwenzio.




Mrembo na mwingizaji, Elizabeth Michael “Lulu” ameweka wazi mtanzamo wake kuhusu simu ya mpenzi wake kwa kusema yeye hawezi kuipekuwa kwani anaiona kama ni bomu.




Lulu aliandika hayo kwenye ukurasa wake kwenye mtandao wa INSTAGRAM mara baada yakuweka picha ya mtoto akilia ikiwa na maadishi ya lugha ya kingereza yakiwa na maana kuwa hiyo ilikuwa ni baada ya kupekua simu ya mwanaume na kupata kile alichokuwa anakitafuta....




Lulu aliiandikia picha hiyo (tazama hapo juu);




“Hii inaitwa MWANA UKOME......Simu Ya Mwanaume naiona kama BOMU...!”




Wewe je simu ya mwenzi wako unaichukuliaje?

Socials