Mwana mama akamatwa akifanya wizi wa mtandao.



Mama ambaye anatuhumiwa kwa wizi wa mtandao.
Huyu Mama anaibaje?
Huyu mama anaanza kwa kutafuta mawakala wa M-pesa na kujitambulisha kwamba ni mfanyakazi wa vodacom na anaonyesha kitambulisho kabisa.
Mbinu anayotumia ni kwamba anawaambia kuna usajiri mpya kutoka vodacom so ametumwa na manager wa vodacom kuja kuwafaamisha mawakal wao, kwahiyo ukimuamini na kushika simu yako umekwisha.
Ataanza kwa kusema ngoja nikuelekeze jinsi ya kusajili,sasa utakapoingiza password, hapo hapo anaikariri haraka halafu baada ya hapo anahamisha pesa na baada ya kuhamisha pesa anakwambia zima simu kwa mda wa dakika 20 ili iji-update kwenye system.
Ukisema umruhusu tu afanye hivyo basi kumbe muda huo anakuwa anatumia kutoa hizo fedha sehemu nyingine.
Lakini jambo zuri ni kwamba kwa sasa anashikiliwa kituo cha polisi kwa mahojiano zaidi baada ya kukamatwa akifanya matukio hayo ya kihalifu.

Socials