
Magazeti Pendwa kutoka Global Publishers yakaamua kumtafuta Gardner ili aweke bayana juu ya suala la ndoa yao kutokana na mwanamuziki huyo kuweka wazi kwamba tayari ndoa yao ilikwishasambaratika.“Alichokisema na ulichokisikia ndiyo ukweli wenyewe. Hakuna ndoa tena, tumekwishaachana na kila mmoja kuchukua kilicho chake. Ila kila kitu namwachia Mungu na wala sina kinyongo naye,” alisema Gardner.
...Wakiwa kwenye pozi. Siku chache zilizopita mwanamuziki Jide alifunguka kwamba hakutaka tena kuendelea kuishi na mume wake kutokana na tabia mbaya alizokuwa nazo mwanamume huyo, hali iliyomfanya kuishi pasipo kuwa na furaha katika kipindi kirefu cha ndoa yao.
Akifunguka zaidi, Jide alisema kwamba alichoshwa na tabia hizo ambazo alipobanwa zaidi ili aziweke wazi tabia hizo, alisema kwamba mwanamume huyo alikuwa na tabia ya kuwashikashika wanawake kila alipokuwa jukwaani akiimba.
Wawili hao walifunga ndoa Mei 14, 2005, jijini Dar es Salaam ambapo mpaka wanaachana, hawakubahatika kupata mtoto.