Mapishi ya pilau la kuku






Mapishi ya pilau la kuku




Kuandaa: dakika 15

Mapishi: dakika 25



Walaji: 5



Ujuzi: Wastani



Gharama: Wastani



Pilau ni mchanganyiko wa mchele na viungo mbalimbali,chakula hiki ni kitamu sana na watu hupendelea sana kupika wakati wa sherehe. Unaweza ukala pilau na kitoweo chochote kile unachopenda mfano mimi nimependa kula na njegere,kachumbali na matunda.












Mahitaji
Mchele
Kuku
Mafuta
Vitunguu maji
Carrots
Pilipili hoho
Tangawizi
Viungo vya pilau
Vitunguu saumu
Chumvi
Nyanya 3


Wapi kwa kupata bidhaa?


Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo
Mkate kuku umpike na chumvi akiiva hakikisha supu ya kupikia chakula inatosha.
Menya vitunguu maji ukatekate,vitunguu saumu menya utwange na tangawizi,menya carrots uzikwangue na pilipili hoho ukatekate mwisho nyanya pia menya ukate kate.
Bandika sufuria utie mafuta, ikichemka tia vitunguu uvikaange. Vikianza kubadilika rangi weka vitunguu saumu na tangawizi mbichi koroga kidoga weka pilipili hoho na carrots.
Kaanga kidogo kisha weka nyanya acha ziive na vipande vya kuku koroga kama dk tano weka viungo vya pilau.
Weka mchele koroga kisha tia chumvi na umimine supu ile ya kuku kwenye wali.
Koroga kisha funika acha chakula chako kiive baada ya dk kumi angalia chakula chako kama maji yamekauka kigeuze palia baada ya dakika kadhaa angalia tena hapo chakula chako kitakua tayari kuliwa.

Socials