HUKU NI KUTUTAFUTA LAWAMA MADEREVA...



Hakika hakuna namna nyingine ya kuelezea kinachoendelea ila kwa maneno machache tunaweza kusema, "Huku ni kutafutana lawama tu!"

Kijana huyu mlemavu anaonekana akiendelea na shughuli yake ya kuomba misaada kutoka kwa wasamaria walioko kwenye magari eneo la Ubungo Darajani, jijini Dar es Salaam.
Ni haki yake, lakini ukweli unabaki kwamba eneo alilochagua kufanyia shughuli yake hiyo sio salama hata kidogo na ni hatarishi kwake na kwa watumiaji wengine wa barabara hususani madereva.
Cha kushangaza ni kwamba, matukio haya yamekuwa mengi sana na zaidi yanashuhudiwa ama kufanyika mbele ya askari wa usalama barabarani ambao wana jukumu la kutoa elimu kwa watumiaji wa barabara juu ya usalama wao na wenzao.
Imekuwa kawaida kwa mamlaka husika kusubiria mpaka janga litokee ndipo wao waweze kutoa tamko badala ya kuwahi kuzuia janga hilo lisitokee.
Mathalani, na hatuombei hilo. Ikitokea kijana huyu akakanyagwa za gari, nani alaumiwe?
Maana ni ukweli ulio wazi kwamba madereva wa malori hawawezi kabisa kumwona kijana huyu anaposota kwenye lami. Isitoshe mawazo yote ya madereva huwa kwenye foleni hasa kutokana na ukweli kuwa wengi wao wanakuwa wameganda humo kwa muda mrefu sana.
Wito: Tunaomba mamlaka husika hasa zile za usalama wa barabarani kuingilia kati katika hili ili kuepusha majanga ambayo yanaepukika kabisa na yaliyo ndani ya uwezo wetu.

Socials