POLISI KENYA WAONGEA KUHUSU GARI LA MBOWE LILILOKAMATWA KENYA

POLISI KENYA WAONGEA KUHUSU GARI LA MBOWE LILILOKAMATWA KENYA

Kwenye magazeti ya April 30 2014 Tanzania miongoni mwa stori kubwa ilikua ni hii ya kukamatwa kwa gari la kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani bungeni ambae pia ni mwenyekiti wa Chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA Freeman Mbowe ambapo baadhi ya vichwa vya habari vilisema ni kutokana na kuhisiwa kutumika kwa ugaidi.

Msemaji wa Polisi nchini Kenya Gatiri Mboroki anaethibitisha kwamba ni kweli gari la Mbowe lilikamatwa tarehe 25 April 2014 ambapo gari hilo baada ya kuvuka mpaka kuingia Kenya likitokea Tanzania lilibadilishwa namba.
Anasema ‘kutokana na visa vya ugaidi nchini Kenya baada ya Wananchi kuona gari imebadilishwa namba na kupaki kwenye hoteli wakaripoti Polisi, Polisi walikwenda na kumkuta dereva peke yake aliewaambia kwamba kiongozi wa chama ambae ni Freeman mwenye gari amekwenda Nairobi kwa ndege, hiyo ilileta utata kidogo kwa kujiuliza amekwenda Nairobi kwa ndege iweje aache gari?’

Socials