Utapeliii!!! HAWA NDIYO MATAPELI WANAOTAPELI WATU KWA NJIA YA MTANDAO KUWA NAO MAKINI SANA HEBU ANGALIA UTAFITI HUU ULIVYOBAINI NA JINSI YA WANAVYOIBIA WATU PIA JINSI YA KUWAEPUKA
TAARIFA HII IMEANDALIWA NA BILL DE PIERREE
Mara nyingi imekuwa kama hulka kwa kuingia facebook na kukutana na sms kama hizi:Hello dear, my name is miss Linda i am so happy to read your profile today in facebook.com please i will like us to know each other and to establish a strong relationship.contact me on (Lindayakoti3@yahoo.co.uk) and to enable me share my picture with you and for you to know me more in further communication.have a nice day. Thank yours lovely Miss Linda.
HELLO DEAR,
I am a beautiful young and charming girl looking for real love,I have gone through your profile,and am very happy to contact you for us to know ourselves,you know that distance,age and indeed color cannot stop true love,i would appreciate if you send mail to my private Email box ( favorsea@yahoo.in )So that i can send my pictures and more information about my self to you,
FAVOR.
na kuna wakati mwingine hawa watu hutumia google translator ili kubadili katika kiswahili na huu ni mfano wa message yao ya kiswahili
Hello jina langu ni Miss Farima (farimahassan2@yahoo.com) Kwa mawazo yangu na moyo wangu aliniambia kuwasiliana na wewe kwa urafiki, tafadhali tafadhali kukubali pedido.Vou yangu kutuma picha yangu na wewe mara moja kupata jibu lako katika email yangu id (farimahassan2 @ yahoo.com) Farima yake adorable.
Hello my name is Miss Farima ( farimahassan2@yahoo.com ) With my mind and my heart told me to contact you for friendship, please please accept my pedido.Vou send my pictures to you immediately receive your reply in my email id (farimahassan2@yahoo.com) her adorable Farima.
watu hawa mara nyingi sana wamekuwa wakifanikiwa kuwtapaeli watu haswa kwa mtego mdogo tu ambao mtu anajikuta ameingia KINGI bila kujua kwani jinsi wanavyokuibia kwa hali ya kawaida kabisa huwezi kugundua lakini huu ni utafiti wangu ambao ilinibidi nijitoe ufahamu na kujua haswa nini lengo lao hawa watu wasioishiwa na matatizo kila siku wao tu ndo wenye matatizo lakini kwangu mimi ilikuwa ni seheu nzuri sana ya utafiti na hali hii ilianza kama ifuatavyo:
Kwa mara ya kwanza nilikutana na message zao kwenye mtandaao ya netlog huko ndiko walikoanzia ingawa kwa mara ya kwanza niliona kama zali vile ki ukweli nilitaka kama vile kuwaamini lakini mwisho wa siku nilichukua hii kaka case of study kwa faida yangu mwenye hawa watu mara nyingi wanapokutumia sms zao na kukupa email zao mara nyingi wanakuambia uwape jibu kupitia email address zao na ukishawapa jibu tu basi wanakupa mlolongo wa matatizo yao anakuambia yeye ni mtoto wa boss fulani ambaye baba yake alikuwa kwnye mapigano ya kikabila huko Rwanda enzi hizo kwa hiyo sasa hivi yupo kwenye kambi ya wakimbizi huko Dakar Senegal na ili kukuvuta zaidi anakutumia na picha yake au wakati mwingine kukuita kwa jina zuri au kukupa ahadi ambayo mtu lazima ushawishike tu kama wewe ni mwanaume utakuta anakuita sweet,love au jina jingine lolote lile tamu ili uzidi kunogewa lakini sasa swali ni kwamba inamaana hiyo kambi inatunza wakimbizi wanawake tu? mbona wanaotuma sms huwa ni wanawake tu?inamaana hakuna wakimbizi wanaume wenye matatizo?cha ajabu kabisa hata hiyo kambi wanayoishi haina jina kamili tungeweza hata kuiserch kwenye mtandao na kujua ilipo au pia inaweza kuwepo lakini ikawa fake pia maana website zinatengenezwa tu
JINSI WANAVYOKUIBIA
watu hawa wamekuwa ni wajanja sana sana anapokutumia email na kukueleza matatizo lukuki basi anabaki kukushawishi kwa donge nono la hela kwamba baba yake aliacha kiasi cha $350million kwnye benki ya dunia kwahiyo anakuteua wewe uwe msimamizi wa hela hizo halafu eti ukifanikiwa kuzichukua basi atakuaj nchi uliyopo na mtaishi kama mke na mume kwa hiyo utafiti wangu haukuishia hapo bado nilienda nao hadi wakanipa namba zao za simu nikawa nawasiliana nao na mimi nikajifanya kweli nashughulikia hizo hela baadae akaniunganisha na mwanasheria wao ambao yupo huko kwa mujibu wa maelezo yao basi baada ya kukabishiwa huyo mwanasheria nikaanza mawasiliano naye ki ukweli ilichukua muda kidogo kama takribani miezi 6 yaaani hapa kama huna akili ya ziada lazima wakulize na tena wizi wao wanakuibia hela ndogo tu sasa jiulize je ni wangapi watakuwa wametuma hizo hela?
baadae wanakuja na sera kwamba hela tayari zimetoka kwa hiyo ili kuzichukua unatakiwa wewe unayefuatilia umlipe mwanasheria kiasi ambacho wanakuw wamepanga kwa wakati ule walianiambia nimlipe mwanasheria wao huyo 100$ ili akamilishe zoezi zima la kuzikomboa hela yaani hapa sasa ndipo wizi unapofanyika kwenye hizo hela za kumlipa mwanasheria na ukiangalia wewe mwenyewe unauchu na hizo 350$million unajua kwamba ukizipata utafanikiwa kumbe ndo unaibiwa kwa hiyo hapo kwenye kuzituma hizo hela za mwanasheria ndipo wizi haswa unapofanyikia usipokuwa makini unaweza kulizwa kwa mimi walipofikia hatua hiyo ya kumlipa mwanasheria zoezi langu likawa limeishia hapo nikapiga kimya nikawapotezea kwa kama muda wa mwezi mmoja hivi mara baadae nikaingia kwenye email yangu nikakuta ujumbe umeandikwa kwamba " ASANTE KWA JUHUDI ZAKO ZA KUWEZA KUACHA MUDA WAKO NA KUFUATILIA HELA ZANGU NAMSHUKURU MUNGU NIMEFANIKIWA KUZITOA KUNA MSAMALIA MWINGINE MWENYE ROHO NZURI KAMA YAKO AMEFANIKISHA ZOEZI HILO ILA KWA SASA HIVI NAENDA KUWEKEZA HELA ZANGU MAREKANI LAKINI PIA KWA JUHUDI ZAKO ULIZOZIFANYA HELA YAKO YA SHUKRANI NIMEMUACHIA MCHUNGAJI GODFREY MWENYE NAMBA ZA SIMU NA EMAIL YAKE NI )zote namba pamoja na email walinipa na nakumbuka walinipa kama 250$million sasa hapa napo kuna wizi mwingine ambao unakuja baada ya kushindwa kukuibia ile awamu ya kwanza baadae nikawasiliana na mchungaji ili nisikie huo ukweli baada ya kuwasiliana na huyo wanae muita mchungaji na yeye akaniambia nimtumie kiasi fulani cha pesa ili aweze kunitumia nikamwambia "sasa kama hela unazo na umenihakikishia kwamba umeachiwa huo mzigo kwa ajiri yangu kwa nini usikate kiasi unachokitaka halafu kilichobaki unitumie?" akaona hapo nimestukia dili akapiga kimya hadi leo hajajibu kwahiyo ndogo zangu hawa watu wanafanya utapeli kijanja sana yaani wananjia zaidi ya moja ya kukuibia wakishindwa njia moja wanahamia njia nyingine.
MATUZI YAO YA FACEBOOK
Siku hizi imekuwa kawaida sana kuingia facebook na kukuta email zao na wengine hata kufungiwa na fb kwa sababu unakuta anatuma sms nyingi kwa watu ambao siyo rafiki zake so facebook huwa wanaamini kwama ile ni account fake ndo maana huwa wanazifunga sasa utajiuliza iweje amenitumia sms leo halafu kafungiwa.
picha zao wakiwa katika pozi mbali mbali za kuwahadaa watu