Sababu 5 Za Harufu Mbaya Mdomoni
Unajiuliza kwanini watu wa karibu
yako wanakaa mbali na wewe kuliko kawaida? Kama wewe ni moja kati ya asilimia
90 ya Waafrica (Tanzania) wanaougua tatizo sugu la kunuka mdomo basi Afya Njema
inakupa sababu za tatizo hilo. Pia Afya Njema tutakupa namna ya kukabiliana na
tatizo hilo.
1. Mdomo mchafu
“Asilimia 90 ya harufu mdomoni
hutoka kwenye mdomo wenyewe – aidha ni kwa chakula unachokula au vijidudu
(bacteria) ambao wapo tayari” anasema Dokta Richard H. Price msemaji wa
American Dental Association. “Harufu mdomoni ni kama harufu zingine za mwili –
ni matokeo ya microbes zinazoishi katika mwili”. Katika mdomo, hii ikimaanisha
bacteria ambao kawaida wanaishi katika mdomo hutumia chakula, damu, na nyama za
midomo n.k kutengeneza (harufu mbaya) salfa (sulfur). Kama husafishi mdomo
sawasawa, bacteria wanajijenga, na kinachofuata harufu mbaya!
2.Mdomo Uliozidiwa kwa Bacteria
Kuna hali Fulani yam domo inaweza
kusababisha bacteria kukuwa na harufu pia, magonjwa ya ufidhi na midomo
kukauka. Magonjwa ya ufidhi (au fidhi) yanasababisha kutokwa damu kwa fidhi,
hivyo kutengeneza mazingira mazuri zaidi kwa hawa bacteria kuwa wengi. Lakini
sababu kuu zaidi ya midomo kunuka ni midomo iliyokauka. Mate yanasaidia
kusafisha mdomo, yanafanya bacteria kutotulia hivyo kuwafanya washindwe
kuzaliana na kukaa sehemu moja, ilhali midomo mikavu ni mizuri sana kwa
bacteria kuzaliana.
3. Vyakula Vinavyonuka
Kama utakuwa chenye harufu mbaya,
kuna uwezekano mkubwa mdomo ukatoa harufu mbaya. Vitu vinavyoongoza kutoka
harufu mbaya ni vitunguu (saumu na maji), pombe na tumbaku.
4. Kula wanga pungufu.
Mlo wenye vyakula vyenye protini
nyingi na wanga (carbohydrates) chache husababisha mwili kuunguza mafuta mengi
yaliyohifadhiwa mwilini ili kupata nguvu badala ya kuunguza wanga na inaweza
kukufanya upate tatizo liitwalo Ketosis. “Karidi mafuta yanavyounguzwa, ketones
zinajijenga kwenye mwili, na zingine hutoka kupitia harufu ya mdomo” anaeleza
Moloo. “Kwa bahati mbaya ketones hazina harufu nzuri hata kidogo.”
5. Kuugua
Mara moja moja, harufu mbaya
huwa ni ishara ya kuugua sana. Magonjwa makuu yanayosababisha kutoa harufu
mbaya ya mdomo huwa ni kisukari au GERD (or gastro osephageal reflux diseas –
magonjwa ya tumbo). Kisukari pia kinaweza kusababisha ketosis, na matokeo ya ya
harufu mbaya mara nyingine huwa ndio dalili za kwanza za kisukari. GERD
(matatizo ya tumbo) ni kurudi kwa aside kutoka kwenye tumbo kwenda kwenye
esophagus. Magonjwa mengine ambayo kwa kiwango kidogo husababisha harufu mbaya
ni magonjwa ya ini au kibofu- hutokea pale sumu kutoka kwenye viungo hivi
kutolewa kuptia mapafu hivyo kusababisha harufu mbaya mdomoni.