RAIS WA UGANDA; ATIA SAINI MSWADA WA PICHA ZA NGONO
Ikiwa unaishi Uganda na unapenda kuvaa nguo fupi, zinazokubana bana au zinazoonyesha sehemu za mwili ambazo zaweza kuwafanya watu wa jinsia nyingine kusisimkwa na kutamani kushiriki ngono nawe, basi jua uko taabuni.
Hii ni kwa sababu rais Yoweri Museveni ametia saini mswada dhidi ya picha za ngono ambao unapinga mavazi yasiyo ya heshima haswa yanayovaliwa na wanamziki na picha za watu wakiwa uchi.