Msafara wa mamba, kenge hawakosi

“Sikufanya shoo za nje lakini kwa hapa ndani nimefanya vizuri sana na nina mshukuru sana Mungu kwa hilo, shoo zote kubwa unazozifahamu nimefanya, hiyo ni sehemu ya mafanikio makubwa kwa mwaka 2013,” anasema Joh


Katika kipindi cha hivi karibuni muziki wa Hip Hop hapa nchini umeendelea kufanya poa sokoni, kutokana na kasi kubwa ya mizuka inayojidhihirisha kwa mashabiki hao.
Hata hivyo, kama wasemavyo wahenga katika ‘msafara wa mamba na kenge hawakosi’ kutokana na malalamiko, kero mbalimbali zinaelekezwa kwa baadhi yao kukosa ubunifu, kuimba nje ya misingi ya Hip Hop pamoja na ‘pumba’ nyinginezo nyingi.
Kauli hiyo inaungwa mkono na mmoja kati ya wasanii wa Hip Hop wanaofanya vizuri katika soko hilo, akijitambulisha kupitia nyimbo zake mbalimbali ikiwemo ya ‘Hao, Chochote, Bye Bye, Sijutii na nyingine kadhaa.
Hapa ninamzungumzia Joseph Simon maarufu kama Joh Makini, Mwamba wa Kaskazini anayewakilisha kundi la Weusi linaloundwa na wasanii wengine kama vile Nikki wa Pili na Gnako.
Joh ambaye kwa sasa anamiliki sanduku lenye zaidi ya nyimbo 40 nje ya kundi lake, anasema pamoja na Hip Hop kuendelea kufanya vizuri, bado kuna baadhi wanaotaka kuharibu.
“Tunategemea kila siku tupate upinzani mkali kwa wasanii wachanga wa Hip Hop wanaoibukia siyo kuimba kwa kutaja taja majina tu ili watu wakusikie, wakufahamu kwa staili isiyokuwa na ubunifu mzuri katika Hip Hop,” anasema Joh na kuongeza;
“Ninachoshauri tu waache kurap rap’, wafanye muziki wa Hip Hop kama unavyotaka, wanatakiwa kuwa wabunifu.”
Hata hivyo, Joh anakiri kuwepo kwa wasanii wakali ambao wataifikisha mbali Hip Hop. “Wengi ambao wanafanya vizuri na ninaamini Hip Hop itaendelea kufanya vizuri zaidi tofauti na watu wanavyofikiria,” anasema John.
Mkakati mwaka 2014
Jambo moja muhimu sana ambalo amepanga kulifanya kama msanii binafsi na sehemu ya Kundi la Weusi, kuandaa video mpya zitakazokuwa na marekebisho makubwa tofauti na miaka mingine.
“Kuna video mpya tunazoandaa kama Kundi la Weusi ambazo ni pamoja na wimbo wa Nje ya Box, G.Wara wara( kolabo na G.nako) na ‘Bei ya mkaa’,” anasema.
Joh ambaye amejijengea utaratibu wa kutoa dozi ya nyimbo mbili tu kila mwaka, anasema bajeti ya kuandaa video hizo inategemeana na mazingira ya uandaaji, gharama ya chini kabisa kwa video moja ni Sh3 milioni ambao haijahusisha vitu vingi.

Socials