WIMBI LA KUIBIWA PASSWORD ZA FACEBOOK ACCOUNTS NA KUTUMIKA KATIKA UTAPELI LASHIKA KASI


Jamani kuweni makini na Accounts zenu za Facebook kwani siku hizi kumeibuka mtindo wa wezi wa mitandao ambao wana iba passwords za Facebook za watu na kisha kuzitumia katika utapeli kwa kuandika status ya kuwadanganya watu na kuwatapeli kwa kupitia account yako....

Nini wanafanya mpaka kupata password yako bila wewe kujua? Kuna njia nyingi wanazotumia kwa mfano hii ni njia moja ambayo hata mimi nimeshajaribiwa kama mara tatu lakini huwa nagundua mapema, Unaweza kuta kwenye inbox yako ya Facebook umetumiwa ujumbe kama huu hapa Chini:
"Habari yako , kuna watu fulani wanasambaza picha zako chafu , ingia hapa kuona hizo picha zako:...Link)"hapo wanakuwekea link ambayo ukiiclick inafungua page kama facebook hivi ila sio facebook na inakuomba Username na Password yako ya facebook sasa wewe kwa vile unataka kuona hizo picha unajikuta umeweka password yako na ukisha submit hakuna cha picha wala nini ila user name na password yako inakuwa imeshatumwa kwa hao wezi na hapo ndio wanaanza kazi ya kutapeli watu ....Mfano wa Message ya utapeli ni hii hapa chini:

NAHITAJI USHAURI WENU GUYS. BE SERIOUS.

Juzi nilikua napitia Ukurasa wa Vodacom Tanzania nikakuta wameweka Tangazo lao la M-PESA lenye hiyo picha wakihamasisha watanzania wajiunge na Taasisi ya Utoaji mikopo iitwayo TANZANIA LOAN ambayo Vodacom wameingia nao mkataba. Hii Taasisi inatoa mikopo bila RIBA.

Nilisoma tangazo lao na kupuuzia nikawa najua ni matapeli hao wametengeneza page feki ya Vodacom nikaipotezea, sasa jana asubuhi nikakuta tena Tangazo katika ukurasa wa ukweli wa msanii Lady Jaydee nae kapewa dili la kufanya matangazo kuhusiana na hawaTANZANIA LOAN pia sikua na uhakika nayo.

Usiku wa jana huo huo nikaona sasa Tangazo rasmi katika TV ilikua TBC1 walirusha Live hilo Tangazo katika Taarifa ya Habari za kibiashara wakatoa mpaka website ya Online mtu anaweza kujiunga na akapatiwa mkopo wa pesa na atarudisha mkopo wa pesa bila kua na RIBA halafu marejesho yao mazuri hawambani mkopaji.

Nikasema ngoja nijaribu kujiunga nione je? Niukweli wanatoa mikopo?? Nikafungua website yao jana usiku http tanzanialoan.wapka.mobi nikasoma maelezo yote! Kuna fomu nikaikuta nikaijaza, nilipoijaza fomu nikapokea ujumbe kua nimefanikiwa kujiunga natakiwa kulipia ada ya Uanachama Tshs. 83,000 (ELFU THEMANINI NATATU ) ili maombi yangu ya mkopo yaweze kuidhinishwa nipatiwe mkopo. Nikawa naogopa kulipia nisije kutapeliwa bure!

Sasa leo Asubuhi kuna jamaa yangu kumbe nayeye ameshawahi kujiunga na wakampatia kweli mkopo nikamuelezea akanitoa hofu! Nikaona kwani elfu83 na kitu gani?? Ngoja nijaribu nikawatumia elfu83 katika M-PESA wakanitumia ujumbe kua wameipokea pesa nisubirie ndani ya dakika30Nikasubiria, kweli wakanitumia mkopo kupitia M-PESA asubuhi hii ya leo muda si mrefu, niliomba mkopo wa Tshs. 3,000,000 (Million 3) hapo nilipo siamini friends.

#USHAURI: Nifungue mradi gani nina hizi Million Tatu, kwani nilikua sijajipanga nilifanya kama najaribu tu sikua na imani kama ntapata kweli huu mkopo nimejaribu wamenipa! Sijajua biashara ipi ambayo inalipa sana?? Please nisaidieni Mawazo yenu nawaomba! Utani tuweke kando nipo serious katika suala hili nahitaji ushauri wenu. Pia kwa yoyote ambae atahitaji kutembelea tovuti ya hawa jamaa wa mikopo, bonyeza hapa: http://tanzanialoanwapkamobi/

Hiyo message hapo mwisho wamekupa link ambayo ukiingia unaambia kama unataka kupata mkopo basi ujaze form na kutuma ada ya sh 83000 kwa kutumia mpesa ama tigo pesa....Ukiingia box ukituma basi imekula kwako hakuna cha mkopo wala nini ...Stuka


Ukiona Message kama hizo wala usiangaike kufungua hizo links ni utapeli mkubwa unaendelea .....

Socials