WAKO WAPI WAKINA MB DOG, Z-ANTO, KEISHA, PINGU, SPARK, DOGO JANJA NA WENGINE WALIYOJITOA TIP TOP??? ZIFAHAMU SABABU ZA WAO KUPOTEA KWENYE GAME..!!

WAKO WAPI WAKINA MB DOG, Z-ANTO, KEISHA, PINGU, SPARK, DOGO JANJA NA WENGINE WALIYOJITOA TIP TOP??? ZIFAHAMU SABABU ZA WAO KUPOTEA KWENYE GAME..!!




Wako wapi MB Dog, Z-Anto, Keisha, Pingu, Spark, Dongo Janja na wengine waliowahi kujitoa Tip Top Connection? Kuna nini Tip Top, kwamba ukijiondoa tu huwezi kufanikiwa mbeleni? Kwanini ni wasanii wachache tu, tena anaweza kuwa Cassim Mganga peke yake ambaye baada ya kujiondoa kwenye himaya hiyo yenye makazi yake Manzese jijini Dar es Salaam, amefanikiwa kuwa na career ya kueleweka? Wengine wote, wamefeli.. big time.

Kinachosikitisha zaidi ni kuwa wengi wakiondoka hutoa maneno ya kashfa na hivyo kujikuta wakinyea kambi.

Hebu tuwaangalia hawa watatu, Dogo Janja, Z-Anto na MB Dog

Dogo Janja

Unakumbuka June 2012, kipindi Dogo Janja ameondoka Tip Top? Habari hiyo ilikuwa kubwa kiasi ambacho simu za Madee na Dogo Janja zilikuwa busy kwa interview. Kila pande ilikuwa ikiutupia lawama upande wa pili.

Kama umesahau wacha tukukumbushe ilivyokuwa.

Sababu zilizotajwa na Tip Top Connection ni kwamba Dogo Janja alilewa sifa na kuwa mtoro shuleni. Kwa mujibu wa interview aliyofanya na Bongo5, uonevu na dhuluma ndivyo vilivyomchosha Dogo Janja kuishi Dar es Salaam na kujiondoa kwenye himaya hiyo.

Alisema tangu aje Dar es Salaam hakuwahi kusaidiwa chochote na Madee zaidi ya mambo ya muziki pekee huku kula, malazi na ada ya shule vikifanywa na rafiki yake Madee aitwaye Abdallah Doka ambaye (Dogo Janja) alikuwa akiishi kwake.

Alisema kutokana na ngoma zake kujipatia umaarufu alikuwa akipata show nyingi nchini na zote alikuwa halipwi chini ya milioni moja. Kilichokuwa kinamsikitisha anasema ni kulipwa hela kidogo isiyozidi laki mbili na hivyo kumfanya aishi kwa tabu licha ya kuingiza hela nyingi za show. “Nilikuwa navumilia tu bro kwasababu kila nilipolalamika kuhusu mambo ya hela Madee alikuwa mkali sana,” aliiambia Bongo5.

Dogo alidai ilikuwa inafikia wakati akifanya show za ukumbuni hulipwa elfu hamsini au chini ya hapo na wakati mwingine alikuwa halipwi kabisa. Alisema tamaa ilizidi kumwingia Madee kiasi cha kumnyang’anya kadi yake ya benki na kuanza kuchukua hela bila kujua password aliipata wapi. “Kuna wakati nilikuwa nataka kumtumia mama laki moja, Madee akanikataza eti kwakuwa watadhani nina hela sana,” alisema.

Aliongeza kuwa kuna siku Madee alimpigia simu na kumwambia kuwa kaka yake wa Kibaha ameandaa show ya CCM na angemlipa shilingi laki moja. “Hivi kweli bro mimi ni mtu wa kufanya show ya laki moja?” alihoji. Hata hivyo aliamua kukubali ili kuepusha lawama.

Baada ya show kumalizika alisema yeye na back up artist wake walirudishwa saa saba usiku wakati asubuhi yake alitakiwa kwenda shuleni kuchukua namba ya mtihani na kuandaa dawati la kukalia. Dogo Janja alisema kuwa ilimuuma sana kwakuwa muziki haujampa chochote licha ya Madee ambaye huwa hapati hata show kumtumia kimaslahi na hadi kufikia hatua ya kujenga nyumba yake.

“Ni kama vile Madee alinipanda ili anivune,” alisema.

Alifunguka kuwa hadi kufikia Tip Top watangaze kumfukuza alikuwa kwa Tundaman akipiga story na Madee akamuita kisha kuanza kumpiga na kwamba alichukua simu yake akaondoka nayo. “Jamaa alianza kujitumia meseji kutoka kwenye simu yangu kwenda kwake za matusi ama kuwa nataka kumroga. Jana nimemuonesha Milard hizo meseji na amesikitika sana.”

Alisema kitendo cha kumwambia Madee kuwa amechoka na anataka kurudi nyumbani ndicho kilimfanya amfanyie yote hayo hadi kumwambia kuwa watahakikisha wanambania asifanye vizuri tena kwenye muziki. Pia amedai kuwa Madee aliwapigia simu wazazi wake ili wamkataze Dogo Janja asifanye interview na vyombo vya habari.

“Wanajua nikiongea wataabika sana.”

Baada ya drama zote hizo ndipo Ostaz Juma akaingia kwenye picha. Alimtumia nauli ya ndege rapper huyo kutoka Arusha kurejea Dar na akajiunga na Mtanashati Entertainment ambayo wakati huo ilikuwa na heshima kidogo. Dogo Janja alipewa maisha, akalipiwa ada ya shule na kutoa ngoma iitwayo Ya Moyoni aliyomshirikisha PNC. Haikupita muda, mambo yakaanza kutokota.

Kwa mara nyingi Ostaz Juma alimfukuza na kumrejesha tena rapper huyo kwa madai kuwa hakuwa na nidhamu. Hata hivyo, imefika wakati ambapo Mtanashati Entertainment imekosa muelekeo na Dogo Janja anahisi meli inazama. Kuomba msamaha ili mambo yaende ni kitu kisichoepukika kwake kwakuwa ni kweli Dogo Janja wa ‘Mtoto wa Uswazi’ ft Godzilla amepotea kabisa.

Z-Anto

Ni ngumu kuamini ukubwa wa Z-Anto baada ya kutoa hit single yake ‘Binti Kiziwi’ ungekuja kuyeyuka kama barafu ikutanapo na jua kali. Enzi Binti Kiziwi inahit, hakuna msanii aliyekuwa na show nyingi kama Z-Anto. Hata hivyo, meneja wa Tip Top Connection aliwahi kudai kuwa kipindi hiki ndipo msanii huyo alianza kuota ‘majipu’ kwapani na kuanza pozi nyingi. Jambo hilo lilimkera Babu Tale kiasi cha kuamua kuifuta kabisa video mpya ya msanii huyo iliyokuwa inategemewa kumpeleka juu zaidi. Baada ya kuondoka Tip Top mpaka leo hii, Z-Anto si yule tena wa zamani na ukweli hali yake kimuziki ni mbaya.

“Nililazimika kushuka kwa sababu hiyo. Lakini nilipokuja kuzigundua zile njia nikaweza kupenya na ngoma binafsi nilijisimamia mwenyewe kwa kila kitu ambayo ndio hiyo Kisiwa cha Malavidavi,” Z-Anto alikiambia kipindi cha Mseto cha Radio Citizen ya Kenya hivi karibuni japo alidai kuwa hadi leo Babu Tale anamtaka arejee kundini.

“Mpaka kesho (Babu Tale) bado ananipenda. Hata ukimuuliza katika wasanii wake anaowapenda atatajwa wawili asishindwe kunitaja mimi.”

MB Dogg

Unazikumbuza Latifa na Si Uliniambia? Hizo ni miongoni mwa nyimbo bora za Bongo Flava za muda wote lakini yuko wapi MB Dogg? Kama ilivyokuwa kwa Z-Anto, naye baada ya kujitoa Tip Top, mambo yalienda mrama. Ilimchukua miaka mingi MB Dogg kuweka ‘ego’ pembeni na kukubali kuwa kweli amepotea na anaiihitaji Tip Top kiasi cha mwaka huu kuweka mambo sawa na Babutale.

“Lakini kwa sasa nataka tumuangalie Mb Dogg kwa macho mawili,” Tale aliiambia Millaayo.com hivi karibuni. Mb Dogg ana kipaji watu wanaujua uwezo wa Mb Dogg, Mb Dogg sio kama amepotea hapana ila hana uongozi anahitaji promo ya nguvu tu akipata hiyo anarudi kupiga hela kama zamani.”

Hata yeye mwenyewe MB hivi karibuni alikiri kuwa kufanya muziki bila kuwa na uongozi wa kukusimamia ni kazi bure.

“Tip Top nilitoka na ndio kitu ambacho kilinirudisha nyuma sana,” MB Dogg aliiambia Bongo5 March 17 mwaka huu.

“Pale nilikuwa nafanyiwa kila kitu, nilikuwa narekodi tu kazi yangu vitu vingine vyote wanafanya wao so baada ya kutoka na kujisimamia mwenyewe nikaanza kuyumba na kuhangaika huku na kule. Kwahiyo kitu ambacho nimegundua msanii bila management nzuri huwezi fika mbali asikwambie mtu. Msanii anahitaji kuongozwa, kushauriwa na mambo mengine. Sasa hivi nipo Tip Top tumeingia makubaliano mapya ya kazi ndio maana nashukuru Mungu ngoma yetu mpya ‘Umenuna’ inasonga kidogo kidogo mpaka kieleweke.”

Kinachowaumiza zaidi wasanii walioondoka Tip Top ni kwamba wasanii waliosalia mathalani Madee, wameendelea kufanikiwa zaidi. Mwaka jana pekee, Madee anadai kuingiza zaidi ya shilingi milioni 150 kwa single yake moja tu ‘Sio Mimi’. Meneja wa Tip Top, Babu Tale akishirikiana na Said Fela ndio walio nyuma ya mafanikio ya Diamond Platnumz, kwahiyo ni wazi kuwa Babu Tale ni ‘hot cake’ kwa sasa na ndio maana wasanii wa Tip Top waliojiondoa wako radhi kumuomba msamaha ili warejee kundini.

Swali ninalokuacha nalo msomaji ni Je! Haiwezekani msanii aliyejiondoa Tip Top kuwa na career yenye mafanikio? -Bongo5

Socials