Sababu 5 Za Harufu Mbaya Mdomoni

Sababu 5 Za Harufu Mbaya Mdomoni



Unajiuliza kwanini watu wa karibu yako wanakaa mbali na wewe kuliko kawaida? Kama wewe ni moja kati ya asilimia 90 ya Waafrica (Tanzania) wanaougua tatizo sugu la kunuka mdomo basi Afya Njema inakupa sababu za tatizo hilo. Pia Afya Njema tutakupa namna ya kukabiliana na tatizo hilo.

1. Mdomo mchafu
“Asilimia 90 ya harufu mdomoni hutoka kwenye mdomo wenyewe – aidha ni kwa chakula unachokula au vijidudu (bacteria) ambao wapo tayari” anasema Dokta Richard H. Price msemaji wa American Dental Association. “Harufu mdomoni ni kama harufu zingine za mwili – ni matokeo ya microbes zinazoishi katika mwili”. Katika mdomo, hii ikimaanisha bacteria ambao kawaida wanaishi katika mdomo hutumia chakula, damu, na nyama za midomo n.k kutengeneza (harufu mbaya) salfa (sulfur). Kama husafishi mdomo sawasawa, bacteria wanajijenga, na kinachofuata harufu mbaya!

2.Mdomo Uliozidiwa kwa Bacteria
Kuna hali Fulani yam domo inaweza kusababisha bacteria kukuwa na harufu pia, magonjwa ya ufidhi na midomo kukauka. Magonjwa ya ufidhi (au fidhi) yanasababisha kutokwa damu kwa fidhi, hivyo kutengeneza mazingira mazuri zaidi kwa hawa bacteria kuwa wengi. Lakini sababu kuu zaidi ya midomo kunuka ni midomo iliyokauka. Mate yanasaidia kusafisha mdomo, yanafanya bacteria kutotulia hivyo kuwafanya washindwe kuzaliana na kukaa sehemu moja, ilhali midomo mikavu ni mizuri sana kwa bacteria kuzaliana.

3. Vyakula Vinavyonuka
Kama utakuwa chenye harufu mbaya, kuna uwezekano mkubwa mdomo ukatoa harufu mbaya. Vitu vinavyoongoza kutoka harufu mbaya ni vitunguu (saumu na maji), pombe na tumbaku.

4. Kula wanga pungufu.
Mlo wenye vyakula vyenye protini nyingi na wanga (carbohydrates) chache husababisha mwili kuunguza mafuta mengi yaliyohifadhiwa mwilini ili kupata nguvu badala ya kuunguza wanga na inaweza kukufanya upate tatizo liitwalo Ketosis. “Karidi mafuta yanavyounguzwa, ketones zinajijenga kwenye mwili, na zingine hutoka kupitia harufu ya mdomo” anaeleza Moloo. “Kwa bahati mbaya ketones hazina harufu nzuri hata kidogo.”

5. Kuugua
Mara moja moja, harufu mbaya  huwa ni ishara ya kuugua sana. Magonjwa makuu yanayosababisha kutoa harufu mbaya ya mdomo huwa ni kisukari au GERD (or gastro osephageal reflux diseas – magonjwa ya tumbo). Kisukari pia kinaweza kusababisha ketosis, na matokeo ya ya harufu mbaya mara nyingine huwa ndio dalili za kwanza za kisukari. GERD (matatizo ya tumbo) ni kurudi kwa aside kutoka kwenye tumbo kwenda kwenye esophagus. Magonjwa mengine ambayo kwa kiwango kidogo husababisha harufu mbaya ni magonjwa ya ini au kibofu- hutokea pale sumu kutoka kwenye viungo hivi kutolewa kuptia mapafu hivyo kusababisha harufu mbaya mdomoni.





Socials