NI SAHIHI KUMUOA X-GIRL WA RAFIKI YAKO WA KARIBU


Nilitokea kumpenda sana binti mmoja lakini sikuwa na uwezo wa kuingia kwenye uhusiano naye kipindi hicho na najua alijua kuwa nampenda lakini kulikuwa na vizuizi flani flani.

Binti alikuwa anakaa hostel ya mabibo na nina rafiki yangu sana walikuwa wanasoma naye baadae akamtokea jamaa kagharamia sana wakawa kwenye uhusiano, na jamaa akaniambia lakini binti hakuniambia coz wote nilikuwa nawasiliana nao, sasa nilionana na binti kanisani na nikamuuliza kuwa najua wapo na uhusiano lakini akaniambia waliachana miezi 6 iliyopita, baadae sanaa siku za mbele nikamuuliza jamaa naye akasema ni kweli waliachana japo jamaa ameongea kinyonge na kwa wasiwasi (nahisi kwa sababu alikuwa anajua nampenda yule msichana na inaonekana yeye bado anampenda sana na yeye ndio alimwagwa).
Basi mimi nikawa nawasiliana na yule binti na kwa sababu nilimpenda siku nyingi nikamwaga sera zangu na binti kanielewa na kwa sasa tumeshaanza rasmi uhusiano japo kimya kimya, kusema kweli natamani kumuoa huyu binti lakini pia namfikiria huyu rafiki yangu, naombeni mnishauri wanangu, je ni sahihi kumuoa binti aliyeachana na rafiki yako wa karibu?

Socials