JINI KABULA: KWA BUSHOKE NIMEKUFA NIMEOZA NAMSUBIRI TUFUNGE NDOA..........!!!!!!!!!

JINI KABULA: NAMSUBIRI BUSHOKE TUFUNGE NDOA



MSANII wa filamu Bongo, Miriamu Jolwa ‘Jini Kabula’ ametoa kali ya mwaka baada ya kusema kuwa hayupo tayari kuolewa na mwanaume mwingine zaidi ya mkali wa Bongo Fleva, Ruta Maxmilian Bushoke aliyeko Afrika Kusini.

Msanii wa filamu Bongo, Miriamu Jolwa ‘Jini Kabula’.

Akipiga stori na gazeti hili, Kabula alisema: “Ndoa yangu itakuwa na Bushoke tu. Sijali umbali wetu, lakini naamini siku moja atakuja na atanioa. Uhusiano wetu uko poa na tunawasiliana vizuri kila wakati,” alisema Kabula na kuongeza:

“Siwezi kusema atakuja lini lakini nawaambia kabisa wanaonizengea, watafute kitu kingine cha kufanya, mimi na Bushoke kilichobaki ni ndoa tu.”

Socials