IKIFIKIA HATUA YA TENDO LA NDOA, BASI EPUKA UVIVU ILI KILA MTU AMRIDHISHE WENZAKE, HUU NDIYO MUONGOZO WAKE.

IKIFIKIA HATUA YA TENDO LA NDOA, BASI EPUKA UVIVU ILI KILA MTU AMRIDHISHE WENZAKE, HUU NDIYO MUONGOZO WAKE.




NITAPENDA kuwa muwazi kuhusiana na hili: tendo la ndoa ni muhimu sana kwa kila mtu awaye yote.Labda Ingekuwa ni vizuri kama tendo la ndoa lisingechukua sura kubwa kwenye mahusiano.

Lakini kwa watu walio wengi, tendo la ndoa ni sehemu kubwa ya mahusiano. Na kwa wanaume, pengine ni muhimu zaidi kuliko ilivyo lazima.

Tendo la ndoa ni ujuzi wa kujifunza. Ni sawa na kuendesha gari, kimsingi mtu yeyote anaweza kufanya hivyo ambapo baadhi yao ni wazuri katika hilo na wengine ni wataalamu kabisaa.

Ila katika hili kila mtu anapashwa afikirie na kujitahidi ili kumridhisha mwenzake na wala sio la upande mmoja kama lilivyo kwa wanaume kuona kama wao ndio wanaopashwa kufikishwa kileleni.

Na mara nyingi malalamiko ya kawaida kwa wanaume ni kukosekana kwa msukumo, kutokuwepo kwa ubunifu wa kucheza hilo sakata, na kukosa mbinu zaidi ya kumfikisha. Na mtu anapokosa kuridhishwa ni kitu ambacho lazima kiwe wazi na ukweli kujadiliwa na wote wawili.
“mwalimu akiwa mbovu na mwanafunzi lazima awe mbovu vinginevyo wakae chini wote wawili kurekebisha. Mwanaume anaweza kusema nimemuacha kwakuwa hawezi kitu Yule!! Je una uhakika kuwa wewe si mbovu?? Bado naweza kusema kwanini swala hili amehachiwa mwanamke peke yake? Maoni yako tafadhali!!

HAYA NI MAANDALIZI YA VYAKULA AMBAVYO VINAFAA KULA KABLA YA KUINGIA KATIKA KAZI MAALUM.
Tatizo la uwezo wa kufanya tendo la ndoa linazidi kukua miongoni wa wanandoa na wapenzi wengi. Takwimu za kitafiti zinaonyesha kuwa karibu ndoa 4 kati ya 10 zenye umri wa miaka 3 na kuendelea zinakabiliana na tatizo hili.

Aidha wanaume 6 kati ya 10 wanatajwa kulalamikia upungufu wa nguvu za kiume na kuacha idadi ya wanawake wanaokabiliwa na tatizo hilo kwa mujibu wa uchunguzi kubaki na asilimia 13.


Pamoja na matatizo mengine kutajwa kuchangia upungufu wa nguvu za kiume na kushuka kwa msisimko wa tendo miongoni mwa wanandoa, uchunguzi umeonesha kuwa utumiaji holela wa vyakula hasa vyenye mafuta ni moja kati ya sababu zinazochangia kwa kasi tatizo hili.

Kwa kuzingatia hilo, watafiti wa masuala ya uhusiano wa kimapenzi wamebaini aina kumi ya vyakula ambavyo vina uwezo wa kumuongezea mtu nguvu ya kufanya tendo la ndoa. Vyakula hivyo ni hivi vifuatavyo:



PILIPILI
Pilipili zilizocheshwa zimetajwa kuwa na uwezo wa kusaidia msukumo wa usambazaji damu mwilini, ambao kwa kiasi kikubwa ndiyo unaoweza kumfanya mtu akawa na hisia kali za kimapenzi. Kwa msingi huo, ni vema kwa wale wanaokabiliwa tatizo la uwezo wa kufanya mapenzi wakatumia pilipili si kwa wingi bali kwa kiwango stahili, ili waamshe hisia zao.

PARACHICHI
Aina nyingine ya chakula ambacho husaidia kuongeza uwezo wa mtu kufanya tendo la ndoa ni Parachichi. Tunda hili linauwezo mkubwa wa kuzalisha vitamini E ambayo husaidia katika uzalishaji wa homoni.

Inatajwa kuwa watu wanaotumia tunda hili kwa wingi huwana msisimko mkali wa kimapenzi na kwa upande wa wanawake husaidia kuongeza majimaji yenye utelezi sehemu za siri na hivyo kuzuia uwezekano wa kuchubuka wakati wa kujamiiana.

NDIZI
Wakati unafikiria uwezo wa kufanya vema tendo la ndoa unatakiwa kuwaza juu ya uimara wa misuli ya mwili ambayo inatajwa kuwa ni sehemu kuu na yenye muhimu katika kujamiiana. Kwa msingi huo ulaji wa ndizi mbivu unatajwa kusaidia kujenga misuli mwilini na kumfanya mtu aweze kuwa hodari katika tendo la ndoa.

CHOKOLETI
Ulaji wa Chokoleti huongeza uchangamfu mwilini na, hivyo kumuwezesha mtu anayeshiriki tendo la ndoa kuwa na mguso sahihi kwenye fikra zake, jambo litakalomuwezesha kupokea hisia za mapenzi kwa urahisi zaidi ya mtu ambaye anakwenda kwenye uwanja wa sita kwa sita akiwa mchovu wa mawazo.

CHAZA NA PWEZA
Aina hizi za samaki zinazovuliwa baharini huwa na madini ya zink na chumvi ambayo yanatajwa kusaidia uzalisha wa vichocheo vinavyohamasisha msisimko wa mwili wakati wa tendo la ndoa.

POMEGRANATE
Ni aina fulani ya matunda mekundu yanayofananana na apple. Haya yatajwa kusaidia kuamsha mishipa ya fahamu na kuweka mawasiliano sahihi ya mwili na hivyo kumuongezea mtu uwezo kwa kufanya tendo la ndoa kwa hamasa kubwa.

MVINYO MWEKUNDU
Mvivyo mwenyekundu unatajwa kuwa na uwezo wa kuuchangamsha mwili na kuongeza msukumo wa damu, kiasi cha kumuondolea mtu uchovu kabla na baada ya tendo la ndoa, hivyo ni muhimu kunywewa hasa na wale ambao wanasumbuliwa na tatizo la kushindwa kurudia tendo.

MBEGU ZA MATUNDA
Mchangayiko wa mbegu mbalimbali za matunda, mfano tikiti, maboga husaidia kuondoa ACID mwilini na kumfanya mtu ajione ni mwenye afya njema.

VANILLA
Vanila husaidia kuamasha hamasa mwili.Mwisho wa aina hizi za vyakula ni TIKITI MAJI ambalo linatajwa kuwa na virutubisho vingi vyenye uwezo wa kuusaidia mwili kuwa na nguvu za kutosha kufanya tendo la ndoa.

Socials