HAKUNA MWANAMKE MZURI ZAIDI YA MKEO


Ni kawaida kusikia Wanaume makazini au mahali popote pale pa mikusanyiko yetu kuwasifia baadhi ya wanawake wanaokatiza mbele ya macho yetu,kitendo hiki hutupelekea wakati mwingine hata kuingia majaribuni
Hili jambo la kumsifia mwanamke ambae umemuona siku moja tu ni kitendo ambacho sikubaliani nacho hata kidogo,mwanamke ambae umemuona siku hiyo tu na ukazuzuka na mguu au makalio tu sio sahihi kabisa
Sidhani kama ulikosea ulipomuona mkeo na najua unaikumbika sana siku ya ndoa yenu
Huyu ni mwanamke uliyemchagua kati ya wana wake zaidi ya Bil 3 walioko duniani
Umemchagua akulelee wanao
Umemchagua akupikie chakula
Umemchagua akupe huduma zote tena katika maisha yako yete
Iweje uwaone wanawake wa mitaani kuwa ndio wazuri??
Unadhani unakuwa unamtendea haki mkeo kweli?
Ukweli ni kuwa hakuna mwanamke mzuri kuliko mkeo dunia yote hii na kutolea macho wanawake wapitaji tu kama hawa sio sahihi
Hao ni wapitaji tu na hicho unachokidhania ni bora kiko kwa mkeo na ni bora zaidi
Hakuna zaidi ya mkeoa na jaribu kumpenda na kumheshimu zaidi
Huyu ndie ubavu wako na hakuna kama yeye
Hebu mpende mkeo na jisikie fahari kuwa nae bana ........!!!!!!!!

Socials