STEVE NYERERE"WASANII WENGI WA BONGO MOVIES HAWAJITAMBUI"

Mwenyekiti wa kundi la Bongo Movie Unity, Steven Mangere ‘Steve Nyerere’ amesema wasanii wengi wa filamu hawajitambui, mbumbumbu na wabinafsi katika kila kitu, jambo linaloleta ugumu katika harakati zao za kujikwamua.
Steve Nyerere ambaye pia ni mwigizaji na mchekeshaji, amesema wasanii wengi wanakosa umoja wa kudai haki zao kutokana na uelewa mdogo walionao huku wengine wakitazama maendeleo yao binafsi.
“Wasanii tumekuwa mbumbumbu wa kila kitu, tumeyumba kwa kuuza na kuibiwa kazi zetu na maharamia. Dada zetu nao wanafanya Bongo Movie ni sehemu ya kufanyia ukahaba.
Pia amesema yeye kama kiongozi anapigania haki za wasanii zisisahaulike katika mchakato wa katiba mpya ili waweze kupata nafuu ya kazi zao.

Socials