NDUGU MDAU WANGU EBU SOMA STORI HII YA UKWELI YA KIJANA MMOJA ALIYEUAWA KWA KUCHOMWWA MOTO BILA YA KUWA NA KOSA.. INAHUZUNISHA YANI ITAKUTOA MACHOZI
Bwana Zimbo (kwenye picha), alikuwa hajaajiliwa kupata kazi tangu alipomaliza chuo, na alishika nafasi ya kwanza kabisa kitaifa katika University of Port Harcourt alipokuwa akichukua degree ya pili.
Alikuwa anahangaika huku akijaribu kumuhudumia mama ya aliyekuwa anateseka kwa ugonjwa wa Kansa ya Ziwa.
Siku kadhaa zilizopita alienda kutafuta dawa katika duka lililo mbali na alipokuwa akiishi ambapo alienda kumtafutia dawa mama yake aliyekuwa anateseka na maumivu ya gonjwa lililokuwa likimsumbua.
Bwana Zimbo alifika dukani na kumkosa mtoa huduma wa duka hilo la dawa ndipo alipofikiria na kuona mama yake anateseka basi akaamua kuingia na kuchukua dawa zenye thamani ya shilingi elfu 9 tu na kuiacha pesa hiyo dukani humo humo.
Baada ya kumaliza kuchukua dawa na kuacha hela ndani alianza kutoka nje akikimbia kuwahisha dawa kwa mama ndipo mtu wa duka la dawa alitokea pembeni na kuanza kupiga kelele za, "mwizi,mwizi,mwiziii...."
Bwana Zimbo alizungukwa na wananchi wenye hasira kali ambao walianza kushusha kipigo kikali bila hata kuuliza mwisho wa siku wakamuwekea tairi la gari shingoni na kumpiga moto mpaka akafa, lakini kabla hajafa kuna jamaa alichukua simu ya Bwana Zimbo na kuiweka mfukoni, ilipokuwa mfukoni ziliingia ujumbe mbili kwenye simu ya bwana Zimbo. moja ikisema "wahisha dawa mama yako amezidiwa sana na amekata kauli fanya uje na usafiri tumuwahishe hospitali"
ujumbe wa pili ulikuwa unasema. "Bwana Zimbo umechaguliwa kuwa Meneja katika kampuni yetu ya mafuta na kazi itaaza siku ya kesho kutwa fanya uje uweze kumalizia taratibu za mwisho uwe kazini".
Hayakupita hata masaa mawili na mama yake Zimbo na ye alipoteza maisha.
Dunia gani hii machozi hayakujificha baada ya kusoma hii kijana amekufa wakati akijalibu kusaidia maisha ya mama ya ke mzazi ambaye naye alikufa kwa kuchelewesha hospital na anakufa akiwa amepata kazi na kupewa nafasi ya juu kabisa.