MSAADA:NAKUFA KWA MAWAZO KWA MESEJI HII NILIYOIKUTA KWA SIMU YA MPENZI WANGU

Mwenzetu nimekoma kuchungulia simu ya mpenzi wangu, Maana nimekuta message moja mpaka sasa nafikiria najiona kama mimi sijui mapenzi ....na nikizubaa ntaibiwa Gal wangu ..ki ukweli sijawahi mtumia msg tamu mpenzi wangu huyo kama hiyo na sina uwezo wa kutunga msg yenye mvuto...Nahisi ntaibiwa na wajuzi wa Mapenzi 
Meseji yenyewe hii hapa chini:


"Ki ukweli Mpenzi , Nakupenda kutoka rohoni na nimevutiwa na wewe kiasi kwamba natamani unipe moyo wako uwe wangu niutunze mpaka siku ya mwisho wetu, Nakuona kama furaha ya maisha yangu toka tuonane ewe malkia, Naomba usiniangushe naona matumaini ya penzi kwako, Nakuhaidi kukupa furaha katika kipindi chote tutakachokuwa pamoja huta juta kuwa na mimi, Nahitaji uwepo wako katika dimbwi hili la Mapenzi"



Mwee Nifanyaje? ..Nimeuchuna sijamwambia kitu ila Roho inaniuma

Socials