Mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Sharon Justice Laiza, mkazi wa Kilimahewa jijini Mwanza amefariki dunia katika mazingira ya kutatanisha baada ya kudondoka ghafla akiwa njiani kueleakea kwa mganga wake aishiye Kiseke, Ilemela Mwanza...
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo lililotokea juzi saa kumi na moja jioni , mwanamke huyo alidondoka umbali wa mita kadhaa kabla ya kufika kwa mganga wake.
Baada ya kudondoka, mwanamke huyo alilazimika kumpigia simu mganga huyo maarufu kwa jina ustaadhi akimtaarifu kuwa amedondoka kabla ya kufika na kwamba anahitaji msaada....
Taarifa zinaarifu kuwa, Mganga huyo alituma vijana wake wakamchukue kwa kuwa yeye hakuwa nyumbani wakati huo. Vijana walifika na kumbeba, lakini kutokana na hali aliyokuwa nayo mwanamke huyo, vijana wale walilazimika kumpigia simu mganga wakimtaka aje haraka kwa kuwa hali ya Sharon haikuwa nzuri....
Akisimulia tukio hilo, mganga huyo alidai kuwa baada ya yeye kurudi nyumbani, hali ya mwanamke huyo ilikuwa ni mbaya zaidi kiasi cha kushindwa hata kuleza shida iliyompeleka kwake.
"Niliporudi hakuweza kunieleza shida yake kutokana na hali yake. Nilimuuliza nikusaidiaje, akasema nipeleke Hospitali ya Mwananchi.
"Tulimpeleka lakini wakasema wao hawana sehemu ya kumlaza wakasema twende Bugando. Pale Bugando walisema alikuwa amebanwa na kifua na miguu ilikuwa imekufa ganzi , hivyo akalazwa.
"Wakati huo alikuwa anaongea kwa shida. Aliniagiza niende kazini kwake ( New Mwanza Hotel ) nikatoe taarifa na kisha nirudi kesho yake asubuhi maana wakati huo ilikuwa ni usiku wa saa nane.
"Kabla sijaondoka, Daktari alinambia kuwa mgonjwa anataka maji.Nikaenda katika duka la Bugando kuangalia lakini wakati narudi nikakuta ameshafariki dunia....
"Baada ya tukio hilo, nilirudi na kutoa taarifa kwa balozi na kesho yake asubuhi tukatoa taarifa kwa serikali ya mtaa na polisi." Alisema mganga huyo
Akiongelea kuhusu uhusiano wake na mwanamke huyo, mganga huyo alidai kuwa amejuana naye alipomfuata akiomba msaada wa kupata kazi.
"Tulifahamiana naye baada ya kuomba nimsaidie apate kazi baada ya kufukuzwa alipokuwa hapo mwanzo. Nilifanya mipango yangu, akapata kazi New Mwanza Hotel. Sikuwahi kumtibu ugonjwa wowote mbali na msaada wa kupata kazi"
Mganga wa jadi ( kulia ) akiwa na vijana waliombeba mwanamke huyo .
Mganga wa jadi ( kulia ) akiwa na vijana waliombeba mwanamke huyo .
Wakiongea na mtandao huu, afisa mtendaji wa Kiseke, bi Hellen Mcharo na mwenyekiti wa mtaa wamethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba mwili huo umehifadhiwa hospitali ya Bugando ukiwasubiri ndugu zake toka Arusha.