WAJANE WANAVYO TESEKA SOMA HII


Mama mmoja mjane alianza kuipata kali ya mwaka baada ya ndugu kuanza kuzichukua na kuzitaifisha mali za
marehemu mme wake.

Hali ile ilimwacha akiwa maskini wa kutupwa huku akikabiliwa na jukumu kubwa la kuwasomesha wanae na kuwapa matunzo mema.

Aliumia sana kwa jinsi walivyoteseka na mmewe kuijenga familia na kupata mali hizo na kuona ndugu wakizitumia kwa anasa na kumwacha akiwa analia na vyombo vya sheria vimpe msaada bila mafanikio.

Mjane yule baada ya kulia kwa muda aliamua kumkabidhi Mungu mzigo huo huku akisali na kusema,

"Mungu wangu!!! wewe ni Mungu wa watu wote hasa sisi wajane, naikabidhi familia yangu mikononi mwako eeeh Mungu. Wewe wajua wanahitaji chakula, elimu, mavazi na hata afya bora. Naomba uwe baba wa familia yangu kwani naikabidhi mikononi mwako nikiamini watapata hivyo vyote"

Miezi machache baadae nyumba ya mama yule ilivamiwa na nyuki wengi, na mama yule alishangazwa kuona nyuki wale hawana madhara kabisa.

Akamwita mtu ambaye ni mtaalamu wa kufuga nyuki akamtengenezea mizinga kumi na yote wale nyuki wakajaa.

Miezi michache baadae mama yule akavuna asali zaidi ya lita 200 na kila lita akaiuza kwa zaidi ya shilingi elfu kumi na tano.

Mama akazidi kumshukuru Mungu kwa muujiza ule kabla ya kwenda shambani kwake na kuona kuna wale nyuki wadogo wakiwa wamezalisha asali ipatikanayo chini ya aridhi na kuvuna zaidi ya lita 100 ambazo bei yake ni mara tatu zaidi ya asali ya nyuki wakubwa.

Mama yule alizidi kumshukuru Mungu na sasa anaishi maisha ya furaha na kila mwaka huuza asali nyingi na amejiajiri na watoto wake wanazidi kupata elimu bora huku wakiwa na maisha ya furaha.

Hakika Mungu hujua jinsi ya kuzitunza familia zake na kuzibariki kwa nyakati tofauti.

Rafiki wa fuledi nakuombea kwa Mungu nawe uwe na afya njema na mafanikio makubwa na katika mwaka 2014 Mungu akufungulie milango ya baraka kwa njia tofauti pamoja na changamoto zinazokukabili kama mjane huyu alivyobarikiwa.

Comment AMEN kama una amini kuwa Mungu ndiye mweza wa yote katika maisha yetu na ataubariki mwaka 2014 na kuwa mwaka wa furaha, amani, uzima na mafanikio katika maisha yako.

Ruksa kushare ila usisahau kulike page yetu

Socials