- Wakati Serikali na wadau wakipinga vitendo vya ukatili wa jinsia likiwemo suala la kurithi wajane, kwa baadhi ya watu wa Kabila la Wasukuma ndiyo utamaduni wao.Katibu wa Mila za Wasukuma Mkoa wa Simiyu, Mayunga Kidoyasi anatoa ushuhuda wa yeye mwenyewe kulazimishwa kumrithi bibi yake ili mali ya ukoo isipotee.Anasema “Babu yangu alifariki mwaka jana, baba zetu wakakaa kikao na kumlazimisha bibi mwenye umri wa miaka 98 sasa achague ndugu yeyote wa kumwoa”.
Kurithi wajane
Akizungumza katika Kijiji cha Mhunze wilayani humo, Rachel Yakobo (55) anasema alifiwa na mumewe, Charles John mwaka 1986 na hapo ndipo ndugu zake walipoleta shinikizo la kumrithi.
“Tulijaliwa kupata watoto wawili na mume wangu wa kwanza, lakini alikuja kufariki kwa ajali ya gari eneo la Kolandoto ambayo hata mimi nilinusurika,” anasema Rachel na kuongeza: “Ndugu zake walilishauri nirithiwe lakini haikuwa hivyo. Nilikaa na upweke hadi mwaka 2001 ambapo niliolewa tena na Joseph Heke anayetoka katika ukoo wa mume wangu, ambaye hata hivyo hatukupata mtoto hadi alipofariki mwaka 2008 ndipo nilipoolewa na kaka yake Mayunga Heke.” Anasema awali hakupenda kuolewa na watu wa ukoo mmoja lakini hakuweza kukwepa kwa kuwa ndiyo mila zao zilivyo.
Hata hivyo kwa mume wake wa sasa, Rachel anasema haoni tatizo kwa kuwa ana msaidia kufanya kazi zilizo nje ya uwezo wake.
“Kwa sasa umri wangu umekwenda mno, siwezi kufanya kazi za nguvu, kwa hiyo huyu mume wangu wa sasa ananisaidia kulima, kukata kuni na nyinginezo,” anasema na kuongeza: