Home »
Uncategories »
HUYU NDIYE MTOTO WA AJABU JIJINI DAR...HIVI NDIVYO VITU VYA KUSHANGAZA ANAVYOWEZA KUVIFANYA
HUYU NDIYE MTOTO WA AJABU JIJINI DAR...HIVI NDIVYO VITU VYA KUSHANGAZA ANAVYOWEZA KUVIFANYA
|
Andrea Marcus |
Mbaya zaidi baada ya kula milo hiyo huwa
haoneshi ameshiba.
Maajabu mengine ambayo yanawashangaza watu wanaoishi naye ni jinsi anavyokula
chakula kwa kumwaga chini kisha kukomba mpaka udongo.
“Sina amani ya moyo, naomba Watanzania wanisaidie, mwanangu
ananiuma sana, hata kujisaidia ni hapohapo, chakula anakula kupita kiasi, kama
nilivyosema hashibi na bado hali kama mwanadamu wa kawaida,” alisema mama wa
mtoto huyo.
Akizungumzia madai ya uchawi, mama huyo, Angelina Marcus alisema
mwaka 2001 alimzaa Andrea katika mimba ya miezi nane kwenye Hospitali ya Taifa
Muhimbili, Dar.
“Nilipofika nyumbani tu, alikuja mwanamke mmoja, akasema amekuja kunipa
hongera. Wakati anaingia alianguka, kichwa ndani miguu nje, alipoamka akaaga
akisema anakwenda kuniletea kisamvu.
“Mama yangu akamwambia mzazi hali kisamvu, kama anataka
akanichinjie bata. Yule mwanamke aliondoka, hakurudi tena,” alisema mama
Andrea.
Aliendelea kudai kuwa, baada ya wiki tatu mtoto wake alianza tabia ya kulia
usiku wa manane.
“Hiyo tabia ya kulia amekuwa nayo miaka yote, tulikwenda kwa waganga lakini
wapi! Tukahamia makanisani kwa wachungaji kidogo mtoto alipata nafuu mwaka
jana.
“Mwezi Novemba tarehe kumi na moja, mwaka jana (2013) yule mwanamke
alikuja hapa nyumbani na kuniambia kuwa, mguu ule ni wangu.“Alikaa chini mimi
nikiwa nafua, akaanza kuniambia ‘mjukuu wangu samahani, nimeona unateseka sana
na mwanao, nataka nikurudishie kwani mimi uchawi sasa basi.’
“Nilishtuka, nikamuuliza bibi unasema nini? Akajibu, ‘n imekuja kukwambia huyu
si mtoto ni picha tu, mtoto wako ninaye mimi nyumbani kwangu na nina watoto
wengi ila wa kwako ananisumbua, bora uje umchukue kesho asubuhi,” alisema mama
Andrea. “Siku iliyofuata nilikwenda kwake, sikumwona mtoto ila cha
kushangaza aliniambia kuwa yeye anajua kuroga lakini hajui kutegua, ana mganga
wake yupo Songea (Ruvuma), atampigia simu aje amtegue mtoto wangu arudi katika
hali ya kawaida,” aliongeza mama Andrea.
Mama huyo alisema kuwa aliporudi nyumbani, aliwaambia wazazi wake kilichotokea
na maneno yote waliyoongea na mwanamke huyo.
wazazi
wa mama Andrea walimuita mwanamke huyo akiwa na mumewe na mtoto wao mmoja,
wakamuuliza kuhusu madai hayo, akaomba msamaha kwa kilichotokea.
Sakata hilo likaenda Serikali ya Mtaa Misigani ambapo mwanamke huyo alikiri
mara ya kwanza na kusema kuwa amempigia simu mganga wa Songea atafika wakati
wowote.“Cha kushangaza alikaa kwa nusu saa na kusema amewapigia simu ndugu zake
wamesema huyo mganga amefariki dunia. Kila mtu alimuuliza amepigaje simu mbona
wamekaa naye na hajatoka nje? Akanyamza,” alisema mama Andrea.
Mama Andrea alisema serikali ya mtaa waliliona sakata hilo ni kubwa na
kuamuru babu wa Andrea (jina lipo) kuchukua barua kuipeleka kwenye Kata ili
kesi ihamie huko.
Mama huyo alimalizia kwa kusema kuwa anashindwa cha kuamua kwani kwa maelezo ya
mwanamke huyo hajui akubali mtoto Andrea si wake au la!